Advertisements

Monday, October 20, 2014

SPIKA MAKINDA AENDELEA NA ZIARA YAKE NCHINI OMAN

Spika wa Bunge Mhe Anne Semamba Makinda akipata maelezo toka kwa Katibu wa Bunge la Oman,Ali Nasser Al Mahrouqi ya namna mfumo wa kisasa wa uendeshaji Bunge ulivyo katika Bunge la Oman.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge Mheshimiwa William Lukuvi akiongea na Spika wa Bunge la Oman Sheikh Khalid Al Maawali.Mhe William Lukuvi ambae pia ni Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Bunge ni miongoni mwa wabunge nane wanaoambatana na Mheshimiwa Spika katika ziara rasmi ya kibunge nchini Oman.
Mhe. Spika Sheikh Khalid Al Maawali akifafanua jambo kwa Mheshimiwa Spika Makinda kuhusu ukumbi wa Bunge la Majlis A'Shura.
Mheshimiwa Spika Makinda akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha Oman TV kuhusu ziara yake.
Mheshimiwa Spika akimkabidhi zawadi ya picha ya mlango wa Zanzibar Spika wa Bunge la juu la Oman Majlis Doula, Mheshimiwa Dr Yahya Al Mandhary.Mwingine pichani ni Balozi wa Tanzania Oman Mheshimiwa Ally Saleh.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe akizungumza na Wabunge wenzake waliomo katika msafara.

3 comments:

Anonymous said...

Sasa Mh. Lukuvi na Mh. Spika walilazimishwa kuvaa vivazi hivyo? Mbona wakija Zanzibar hawavai kama hivyo basi?

Anonymous said...

Huyu Lukuvi si ndie aliesema waarabu watarudi Zanzibar na kwamba uhusiano wa Zanzibar na Oman utahatarisha Tanganyika kwa uislam. Nyie vipi mbona hamueleweki. Roho mbaya Sana kwa Zanzibar!!!!. Sasa weye huogopi magaidi hapo?. Wala papo, wanya papo.

Anonymous said...

baniani mbaya kiatu chake dawa..