Advertisements

Sunday, October 26, 2014

TASWIRA ZA TUKIO LA NAIBU WAZIRI WA AFYA WA ZAMANI NA MWANAE

Gari la Polisi likiwa eneo la tukio katika ofisi za Faraja Trust Fund zinazomilikiwa na Mbunge wa Morogoro Kusini, Mh Lucy Nkya, ambapo imetokea tukio la kurushiana risasi baina ya mbunge na mtoto wake, jana asubuhi Jumamosi Oct 25, 2014
Mtoto wa kwanza wa mbunge, Jonas akihojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo.
Mhe Dr Lucy Nkya Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki.
Mhe Dr Lucy Nkya akizungumza na Waandishi wa habari muda mfupi uliopita ofisini kwake Faraja.

Morogoro.Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Lucy Nkya amesema kuwa milio ya risasi iliyosikika ofisini kwake, ilitokana na mtoto wake Jonas Nkya, kuangusha bastola kwa bahati mbaya.
Nkya alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusikika kwa milio ya risasi ofisini kwake huku kukiwepo kwa taarifa kwamba alivamiwa na mtoto wake huyo akidaiwa kutaka kumuua kwa kumpiga risasi.
Taarifa hizo zilidai kuwa mbunge huyo alikuwa na ugomvi wa kifamilia na mtoto huyo aliyefika katika ofisi za Faraja Trust Fund akiwa na bastola kwa lengo la kumuua.
Mbunge huyo aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, alisema kuwa hawana ugomvi wowote na mtoto wake na iwapo wangekuwa na ugomvi angewatumia wazee na wakubwa wa familia kusuluhisha.
“Jonas amehamia nyumbani kwangu kwa ajili ya kunisaidia kumlea baba yake ambaye ana tatizo la kupooza. Kama tungekuwa na ugomvi, tungegombana nyumbani na siyo ofisini,” alisema Lucy.
Alitoa ufafanuzi kuwa Jonas alifika ofisini kwake kwa lengo la kuchukua gari kubwa ili aende shamba, lakini wakati akitoka ofisini humo, aliinama na ghafla bastola aliyoiweka kiunoni ilidondoka na risasi kuanza kufyatuka.
Dk Nkya pia alikanusha taarifa zilizodai kuwa katika ugomvi huo alikuwa akirushiana risasi na Jonas akisema kuwa, binafsi alishika silaha mara ya mwisho mwaka 1972 alipokuwa katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mafinga aliposhiriki zoezi la shabaha.
Alisema kuwa tukio hilo limezua taharuki kubwa kwenye familia yake na kwa viongozi wenzake wakiwemo wabunge pia kumfanya ashindwe kufanya kazi zake. Kwa upande wake Jonas Nkya, ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM, alikiri kufika ofisini kwa mama yake akiwa na bastola akieleza kuwa alikwenda kuchukua gari ili aende shamba na kwamba hakuwa na dhamira ya kufanya shambulizi lolote kwa mama yake kwani hawakuwa na ugomvi.
Alisema kuwa risasi zilifyatua baada ya kuanguka kwa bastola hiyo aliyokuwa ameiweka kiunoni na baada ya tukio hilo alikwenda katika Hospitali ya St Mary kwa ajili kupatiwa matibabu kutokana na mshtuko alioupata baada ya risasi kufyatuka.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa uchunguzi zaidi unafanyika ili kujua kama risasi hizo zilifyatuka kwa bahati mbaya ama kwa nia ovu. “Pamoja na uchunguzi, tunamtafuta Jonas kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusu tukio hilo,” alisema .
Habari na Mwananchi

4 comments:

Anonymous said...

laana ya mzee nkya itawangamiza mpaka kifoo.wamemfanya mzee zezeta ili wapate ustawi katika siasa na biashara matokeo yake wameishia kufarakanisha familia.watoto hawaelewani,biashara zimebuma,na upepo wa siasa nao mmemkalia mama vibaya,faraja trust inapumulia mashine madeni ndo wimbo

usibane mkuu hii kitu watu lazima wajue ndo kueliisha huku

Anonymous said...

laana ya mzee nkya itawatafuna milele malipo ni hapa hapa duniani.

Anonymous said...

Kisa mtoto anataka kiti cha ubunge cha mamake...
wamachame noma sana kwa mali.
na mkuu huyu kishawatapeli na kuwaliza wengi tu kwa udalali wa magari yanayotoka japan

si wangemalizana tu next time waje kwenye shooting range yangu niwafundishe kushoot on target na ku aim katika kichwa na kifua.

Anonymous said...

mambo mengine ni aibu tu. Hii kali ya mwaka mama na mwana.

chezea wa machame wewe kwa mali.Bado hawajauwana tuu.si wangeuwana tu ili kupunguza idadi ya population hapa nyumbabi Tanzania.

wanao hubiri hii ni nchi ya amani,ndio hao hao wanashinda na siraha kiunoni za moto na kivita.

Hakuna risasi tatu zinaweza kutoka katika mguu wa kuku (bastola)kwa bahati mbaya au kuanguka bila ya kukokiwa au kutekenywa trigger.Msitufanye watoto tunazijua silaha Vizuri sana.Kamwe silaha haiwezi kuanguka na kujifyatu yenyewe bila kukokiwa au kuchezea trigger.Never.