ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 21, 2014

Tisa wawekwa chini ya karantini kwa Ebola

Waziri wa Afya, Seif Rashid

Watu tisa wamewekwa chini ya karantini kutokana na kumhudumia mtu anayedaiwa kufariki kwa ugonjwa wa Ebola katika hospitali ya wilaya ya Sengerema, Mwanza mwishoni mwa wiki.

Idadi hiyo imefikia baada ya wafanyakazi watatu wa halmashauri ya wilaya ya Sengerema waliohusika kuuzika mwili wa mgonjwa huyo, Salome Richard (17), kuzuiwa kuchanganyika na wanajamii hadi vipimo halisi vitakapothibitisha ni ugonjwa gani uliomuua msichana huyo.

Salome alifariki usiku wa kumkia Jumamosi akiwa na dalili za Ebola na kusababisha waliomtumia usimamizi maalum na watu kutoka Idara ya Afya waliopo chini ya Halmashauri ya wilaya.

Mwili wa marehemu huyo alizikwa juzi katika makaburi ya Nyampurukano mjini Sengerema chini ya uangalizi wa watumishi wa idara ya afya waliovaa mavazi rasmi.

Mmoja wa wauguzi wa hospitali ya wilaya Sengerema, alisema idadi ya waliowekwa chini ya karantini hiyo imefikia idadi hiyo baada ya wahudumu watatu walioshiriki kuuzika mwili huo kuwekwa chini ya uangalizi maalum hadi majibu ya ugonjwa uliomuua Salome yatakapotolewa na wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikillo (pichani), amewatoa hofu wananchi wa mkoa huo kuhusu kuwapo ugonjwa huo huku Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa, Dk. Yusuph Bwire, akisema wanasubiri sampuli za vipito kutoka ajibu ya vipimo vya awali vilivyotolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili.
CHANZO: NIPASHE

No comments: