Friday, October 3, 2014

UBABAISHAJI WA VIONGOZI WA TIMU ZA TANZANIA UNAWEZAJE KUMNUNUA MCHEZAJI KWA PESA NYINGI BILA KUPIMWA NA KUJUA KAMA ANATATIZO KABLA YA KUSAJILIWA?

Mchezaji wa timu ya Simba, Paul Raphael Kiongera.

Daktari huyo amesema kama Kiongera amekuwa na ugonjwa sugu wa goti, ni nadra kama atanusurika kufanyia upasuaji.

“Ugonjwa wa goti una mambo mengi, siwezi kusema kila kitu kwa kuwa majibu ya tatizo la Kiongera sijayaona.
“Kama ni ugonjwa sugu, asilimia kubwa ni upasuaji na mara nyingi inakuwa ni nje ya nchi,” alisema daktari huyo bingwa.

“Lakini bado inawezekana hata hapa nyumbani ingawa mara nyingi watu hukwepa tu gharama lakini nje ni sahihi,” alifafanua zaidi.

Alipoulizwa jana daktari wa Simba, Yassini Gembe alisema alikuwa mazoezini. “Niko mazoezini siwezi kuzungumza lolote,” alisema.

Taarifa nyingine zikaeleza Kiongera atakaa nje kwa wiki sita ambao ni muda wa mwezi mmoja na nusu.
Hata hivyo, majibu ya daktari aliyempima ndiyo yatakuwa ya mwisho na kuamua kuhusiana na wapi atibiwe.

Kiongera aliumia katika mechi dhidi ya Coastal Union akiwa ameingia kuchukua nafasi ya Amissi Tambwe.

No comments: