ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 1, 2014

ZAMBIA, TANZANIA, KENYA ZASAINI MKATABA KUONESHA DHAMIRA YA KUJENGA MIUNDOMBINU YA UMEME

Mawaziri wanaoshughulikia Nishati kutoka nchi za Zambia, Tanzania na Kenya wakisaini Mkataba wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi hizo kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo.
Mawaziri wanaoshughulikia Nishati kutoka nchi za Zambia, Tanzania na Kenya , Waziri wa Wizara yaMigodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia , Christopher Yaruma (kushoto) Waziri wa Nishati na Madini , Profesa Sospeter Muhongo Tanzania (katikati) na Waziri wa Nishati na Petroli Kenya, Davis Chirchir (kulia) wakibadilishana Mkataba wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi hizo kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo mara baada ya kusaini.
Mawaziri wanaoshughulikia Nishati kutoka nchi za Zambia, Tanzania na Kenya , Waziri wa Wizara ya Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia , Christopher Yaruma (kushoto) Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo Tanzania (katikati) na Waziri wa Nishati na Petroli Kenya, Davis Chirchir (kulia) wakionesha Mkataba wa Makubaliano mara baada ya kusaini.
Sehemu wa wadau waliohudhuria hafla ya kusaini Mkataba wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi za Zambia, Tanzania na Kenya kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo. Mbali na Wataalamu kutoka katika nchi hizo, hafla hiyo imehudhuriwa uwakilishi wa COMESA, Mashirika ya Umeme kutoka nchi hizo na baadhi ya washirika wa Maendeleo wakiwemo Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Ubalozi wa Norway, Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), African Development Bank (AfDB), Ubalozi wa Ufaransa.

No comments: