ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 30, 2014

Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai afanya mazungumzo na Balozi Mdogo wa Saudi Arabia Dubai

Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga amekutana na Balozi Mdogo wa Saudi Arabia, Dubai, ambaye pia ndio Mkuu (Dean of Diplomatic Corps) wa Mabalozi Wadogo waliopo Dubai, Mhe. Emad A. Madani katika ofisi za Ubalozi Mdogo wa Saudi Arabia.

Mhe. Mjenga alienda kumtembelea ili kuomba ushiriki wake pamoja na Mabalozi Wadogo wote kwenye kongamano la uwekezaji kwenye sekta ya Utalii nchini Tanzania, litakalofanyika tarehe 17 Disemba 2014.

Mhe. Emad Madani amesema atashiriki vikamlifu kwenye kongamano hilo huku akisema kuwa Tanzania na Saudi Arabia ni nchi rafiki wa siku nyingi, na hivyo basi wapo tayari kuomba taasisi ya utalii ya Saudi Arabia kushiriki pia.
Aliahidi kuwaomba Mabalozi Wadogo wote washiriki.

Kongamano hilo limeandaliwa na Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Dubai kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

No comments: