ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 30, 2014

ELIMU HAINA MWISHO...BRIG GEN (RTD) ALAMBA NONDO ZA SHERIA LLB CHUO KIKUU HURIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 74

Generali Mstaafu P.S.Ligate Baba Mzazi wa akina Phanuel, Obed, Vupe na Guy Ligate akiwa Mwingi wa Furaha na Mkewe Mama Ligate Baada ya Kutunukiwa Shahada ya Sheria LLB Kutoka Chuo Kikuu Huria (Open Univeristy of Tanzania) Jijini Dar-es-Salaam Weekendi hii.
Generali Mstaafu Ligate alianza masomo yake hayo kama changamoto tu baada ya kuhitimu madarasa yote ya BSF Bible Study na kujikuta bado anapenda kusoma na kujiweka busy akiwa kama mstaafu. Pamoja na umri wake kuwa mkubwa na kusumbuliwa na Magonjwa mbalimbali ya Kisukari na Pressure, Mzee huyu alijitaidi sana na kuonesha umakini mkubwa akiwa masomoni na mwisho alifanikiwa kumaliza masomo yake na kuhitimu wakati wa mwafaka huku akitunukiwa LLB with Upper Second Class. Wanafamilia wanampongeza sana kwa kuonesha mfano kwa Wazee, Wastaafu na jamii kwa ujumla kuwa ule msemo wa Elimu haina mwisho ni Kweli