ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 21, 2014

FM ACADEMIA 'WAZEE WA NGWASUMA' YAMOTO BAND NA BARBANAS KUWASHA MOTO USIKU WA ONYESHO LA 'USIKU MWEUPE' JIJINI DAR


Na Mwandishi Wetu.
 FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' Yamoto Band na Barbanas, kesho watakuwa na onesho maalum liitwalo 'Usiku Mweupe' litakalofanyika kwenye ukumbi wa Escape One, uliopo mikocheni Dar es Salaam.
Mratibu wa onesho hilo Wiliam Malecela, alisema kuwa kila kitu kipo vizuri ambapo onesho hilo litaanza saa 3, usiku.
Alisema kuwa dhumuni la kufanya onesho la pamoja kwa bendi hizo na msanii huyo anayefanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya ni kutaka kuuinua muziki wa dansi ambao umeonekana kufifia.
Malecela alisema kuwa katika usiku huo mweupe umeangalia umri wa kila mdau wa muziki, kuanzia miaka 18 mpaka 50 kwa sababu kuna muziki wa kizazi kipya na bendi ya muziki wa dansi.

 "Kwanza tumeangalia muziki wa dansi kama unapotea ni bora tuanze kuurudisha kwa kufanya onesha la pamoja na vijana hawa ambao kwa sasa ni moto wa kuotea mbali, vile vile tumeamua kuunganisha watu wa lika lote waje kushuhudia burudani safi"alisema Malecela.
Alisema ana amini kila mpenzi wa muziki atapata burudani safi na kukumbuka usiku huo maalum.
Malecela alisema kuwa wamejipanga kwa kuweka ulinzi wa aina yake, ambapo kila atakayekuja atakuwa salama.

 Mkurugenzi wa Blog ya Wananchi, William Malecela akiongea wakati wa onesho maalum liitwalo 'Usiku Mweupe' utakaofanyika ukumbi wa Escape One jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Serengeti Platinum, Elihuruma Ngowi (Kati) akiongea machache.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
 Waandishi wa Habari.
"Tumejipanga kila sehemu hata suala la ulinzi, tumeomba kupata ulinzi wa kutoka, kwa kila atakayekuja atapenda, maana atakaa mpaka anaondoka akiwa yupo vizuri"alisema Malecela.
Alisema katika onesho hili viingilio ni shilingi 20,000 na 10,000.
Limedhaminiwa na Serengeti Platinum, CXC Africa,Clouds FM,Jambo Leo, Smart, Blogu ya Wananchi, Udaku Special na Domo Cosmetics.

3 comments:

Anonymous said...

le mutuz le professor le bigshow umetuvalia mawani tusikuona sura yako haya bwanaaa.

Anonymous said...

naskia le mutuz aliishi marekani miaka 30 na alikuwa na degree 3o na alikuwa na degree 3 na master 1 ni kweli.nakumbuka mimi nilivyokwa na chapuka kupata degree yangu ya mwanzo alikuwa ananishanga shangaa nikasoma mahali ana degree hizo na master nikashanga naombeni wanao mjua mtufahamishe please.

Anonymous said...

Mwanga mkubwa wee...maind your own business.