Advertisements

Friday, November 21, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA PILI WA KIMATAIFA WA LISHE NA VIRUTUBISHO (ICN2) ROME ITALIA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib  Bilal, akihutubia Mkutano wa pili wa Kimataifa kuhusu Lishe na
Virutubisho (ICN2) uliofanyika katika ukumbi wa Makao Makuu ya Shirika
la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) jijini Rome, Italia juzi
Novemba 19, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib  Bilal, akijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wakati wa mkutano huo wa ICN2 (kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Italia,  James Nsekela na Msaidizi wa Rais katika Masuala ya Lishe Dkt. Wilbald  Lorri.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango Maalum wa Chakula Duniani (WFP) Ethria Cousin (kushoto) na Balozi Wilfred Ngirwa  wakati wa mkutano huo wa ICN2, uliofanyika juzi Novemba 19, 2014, Jijini Rome Italy.
 Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akifuatilia hotuba mbalimbali za viongozi
walioshiriki katika Mkutano huo wa ICN2. Kulia ni Mfalme Letsie III wa
Lesotho.
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi
Mtendaji wa FAO Jose Graziano da Silva, wakati alipomtembea ofisini
kwake na kufanya naye mazungmzo, juzi Novemba 19, 2014. Kushoto ni
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid. Picha na OMR.

1 comment:

Anonymous said...

MHESHIMIWA MAKAMU DKT BILAL, Mimi mdau naona ukifika huo muda uende moja kwa moja kuchukua fomu yako ya kuomba kuingia kinyanganyiro cha urais ila usiwaonee huruma wale wafisadi na wala rushwa!!