Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiongea ofisini kwake wakati akikabidhi Vifaa mbalimbali kwa wananchi wa Jimbo la Morogoro Mjini Ikiwa ni Utekelezaji wa Ahadi zake alizotoa Kipindi Akiomba kura ya Kuwa Mbunge wa Jimbo Hilo Pamoja za Ahadi anazotoa kwenye Mfululizo wa Ziara zake anazofanya Mara kwa mara katika Kata Mbalimbali za Jimbo la Morogoro Mjini.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood akikabidhi Mbao kwa Viongozi wa Msikiti kwajili ya Kumalizia ujenzi wa Msikiti ikiwa ni ahadi aliyoitoa wakati wa ziara zake za mara kwa mara.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akikabidhi Tani 2O za Saruji kwa viongozi wa Kanisa la agae la Mjini Morogoro Kwajili ya kufanikisha Ujenzi wa Kanisa Hilo.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akimkabidhi Tank la Maji Diwani wa kata ya Bigwa kwa niaba ya wakati wa kata hiyo Ili kutatua kereo ya Maji katiaka kata hiyo
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akikabidhi Hundi ya Shilingi Laki Tano kwa kikundi cha wa mam wajasiriali Kutoka kata ya Kihonda Magorofani
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akikabidhi Hundi
Katika Shuguli yake ya kukabidhi Vifaa mbalimbali Mh Abood alikabidhi vifaa vyenye Jumla ya Shilingi Milioni 1756OOOO/= Katika vikundi Mbalimbali vya Wajasiriamali,Vya Kidini kutoka kata za Jimbo la Morogoro Mjini.Baadhi ya Vifaa alivyokabidhi Mh Abood ni amoja na Matofali ,Vifyuko ya cement,Mabati Mbao na Hundi.
Akielezea zaidi Mh Abood alisema Maka sasa ameweza Kuchimba Visima 24 Kati ya 36 Vitakavyogharimu Kiasi cha Shilingi Milioni 365. Karibu kata Zote za Manisaa ya Morogoro Kwasasa Zina Kisima Kwajili ya kutatua changamaoto Kubwa ya maji inayowakumba wakazi wa Jimbo la Morogoro Mjini.Akielezea zaidi Mh Abood Alisema Anapambana usiku na Mchana kutatua Kero Zote zinazowakumba wananchi wa Jimbo la Morogoro Mjini..
Akielezea Utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na Ahadi zake alizotoa kwa wananchi wa jimbo la Morogoro Mjini Mh Abood Amesema karibu ahadi zake zote alizoahidi Amezitekeleza ,Amewaomba wakati wa manisaa ya Morogoro Kushikiana nae Bega kwa Bega katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mainduzi.
3 comments:
Achene kutudanganya kwenye chaguzi zinapokaribia ili muendelee kuikamua Tanznaia na walipa kodi ili kujinufaisha wenyewe! kwani kama ni kutoa sementi siku zote mlikuwa wai kama ingekuw ainatolwea hata mifuko ishirini kila baada ya miezi sita si tungeendeleza sehemu nyingi saan ukizingatia shule zetu zisokuwa na milango!! Fikiria ni majengo mangapi umejenga wew mwenyewe kipindi chote cha uchaguzi uliopita??? achene hizo??
Mzee asante sana lakini kwa kweli kama sio kufunganisha macho wa wadau ni nini. Kauli ya kusema kumaliza tatizo la maji inalenga penyewe kweli yaani tangi moja la kuhifadhia maji linamaliza tatizo la maji mkoa mzima. Na sisi viongozi tunaowatumikia wananchi waliotuchagua ngazi za chini tunafanya makosa kuwabembeleza walio juu yetu kwa vizawadi vidogo na kuonekana kuwapokea wajapo kwenye maeneo. Tujifunze kuwaambia ukweli sio kujidanganya jamani nchi haitaendelea kwa jinsi hii. Ridhiwani juzi katoa msaada wa baiskeli ni kitu kidogo saan tofauri na anayopata ikifpia uchaguzi hizo baiskeli mtaendelea kulipa kuzifanyia matengenezo wakati yeye anatanua!!tujipeni poleeeh.
Mr Abood una uwezo wa kutosha sidhani kama nafasi ya kuwahudumia wananchi upo ndani ya moyo wako. Fedha ulizo nazo ndizo zinakupa nafasi hiyo! kama ndio hivyo kweli fanya bali usingoje kipindi cha uchaguzi ujionyeshe kutoa huduma zaidi, uwezo unao na unaweza kufanya fanya kabla ya chaguzi unaweza!!
Post a Comment