Advertisements

Wednesday, November 26, 2014

RIPOTI YA GAG KUHUSU AKAUTI YA ESCROW YAWASILISHWA BUNGENI LEO

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mhe Zitto Kabwe akisoma Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (GAG) kuhusu akauti ya ESCROW Bungeni Mjini Dodoma leo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akifafanua jambo wakati akiendesha Bunge hilo leo mjini Dodoma.
Baadhi ya wahudumu wa Bunge wakigawa Ripoti ya GAG kuhusu akauti ya ESCROW kwa Wabunge
Waheshimiwa Wabunge wakipitia ripoti ya GAG kwa makini wakati ikisomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe Zitto Kabwe.

Waheshimiwa Wabunge wakimsikiliza Mhe. Zitto Kabwe (hayupo pichani) wakati akisoma ripoti ya CAG.
Baadhi ya wahudumu wa Bunge wakigawa Ripoti ya GAG kuhusu akauti ya ESCROW kwa Wabunge
Waheshimiwa Wabunge wakipitia ripoti ya GAG kwa makini wakati ikisomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe Zitto Kabwe.
Baadhi ya waandishi wanaoripoti habari za Bunge wakifuatilia mjadala kwa makini.
Naibu katibu wa Bunge, John Joel akijadiliana jambo na Mhe. Spika Anna Makinda.
Wabunge wakiwa wamesimama kuashiria kuunga mkono taarifa iliyosomwa Bungeni leo na Mhe. Zitto Kabwe.
Mhe Said Arfi akimpongeza Mhe.Zitto Kabwe ,mara Baada ya kumaliza kusoma ripoti ya GAG.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,Mhe DEO Filikunjombe akiwasilisha maazimio ya kamati yake.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirisha Bunge mpaka kesho ambapo Serikali inatarajiwa kutoa majibu.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mhe. Stephen Masele akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Bunge kuahirishwa. Picha zote na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii kanda ya kati

1 comment:

Anonymous said...

Kwa wale tulioisikiza Taarifa hiyo inadhihirisha how quickly we are likely to generate into a Mafia State. That Chenge continues to be a king maker and author of our proposed constitution is unbelievable!!