Wananchi wakishuhudia basi la Wibonela lililopinduka leo asubuhi huko Kahama.
Wananchi wakiwa eneo la ajali huku wengine wakijaribu kupata picha za hapa na pale
Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi uliopelekea dereva wa basi kushindwa kulimudu lilipofika kwenye kona ya Phantom na kupelekea kuingia mtaroni na kupinduka.
Idadi kamili ya waliopoteza maisha na majeruhi kwenye ajali hiyo bado haijafahamika.
Baadhi ya miili tayari imetolewa katika eneo la ajali huku majeruhi nao wakikimbizwa kwenye Hospitali ya Wilaya Kahama kwa matibabu.
No comments:
Post a Comment