Advertisements

Monday, November 24, 2014

TUCTA WAIBUKA WASEMA LIWALO NA LIWE WAMECHOKA SOMA HAPA KUJUA KULIKONI



Pichani ni Rais wa mpya chama cha Wafanyakazi nchi TUCTA Gration Mukoba picha na Maktaba
Na karoli Vinsent
CHAMA cha Wafanya kazi nchini (TUCTA) nao wamejitosa Kwa mara ya Kwanza kwenye sakata la Ufisadi wa zaidi ya bilioni 400 za kitanzania kwenye Akaunti ya Escrow na kusema chama hicho hakiwezi kukubaliana na ufisadi huo na kuitaka serikali kuwachukulia hatua kali ya watu wote waliohusika na wizi.
Na kama endapo Bunge pamoja na serikali hawatawachukulia hatua zozote Viongozi waliohusika na wizi huo, basi TUCTA itachukua Jukumu la kuwaunganisha wakulima na wafanyakazi wa idara zote kushikilia bango suala hilo.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar Es Salaam na Rais Mpya wa Chama cha Wafanyakazi nchini TUCTA Gration Mukoba wakati wa Mkutano na waandishi wa habari, ambapo Mukoba alisema wao TUCTA ambao nao pia ni walipa kodi nchini hawawezi kukubaliana na wizi wa zaidi ya Bilioni 400 kwenye Akaunti ya Escrow.

“Kusema kweli sisi wafanyakazi tumechoka na hali ya Ufisadi unaoendelea nchini, na ukizingatia sisi TUCTA ni walipa kodi wakubwa sana ,tunasikitika sana kusikia serikali inaweza kusimamia mambo ya ufisadi yanayotokea maeneo mbalimbali nchini, na sisi vyama vya Wafanyakazi nchini kwa pamoja tunaiomba serikali iwachukulia hatua kali sana Viongozi waliohusika kwenye wizi huu wa mali za umma”alisema Mukoba.
Mukoba aliongeza kuwa kwamba wafanyakazi nchini wanaishi katika mazingira magumu sana huku wengine bado wakiwa wananchukua mashahara mdogo ambao usioendana na hali ya maisha ya sasa na wanasikitika kusikia pesa zinaibwa na watendaji wa serikali na huku wakishindwa kuchukuliwa hatua.
Aidha Mukoba aliwashangaa watu ambao wanasema pesa ambazo zimeibwa kwenye Akaunti ya Escrow kusema sio za umma bali ni za wamiliki wa Kampuni ya IPTL na kusema sio kweli kwani pesa hizo ni za watanzania wote, kwani zimechukuliwa kwenye shirika la Umeme nchini Tanesco.

Vilevile TUCTA wameiitaka Jamii kujiweka Tayari kuungana nao ili kuchukua maamuzi magumu kuhusu ufisadi huo na kama endapo Serikali itashindwa kuwachukulia hatua Viongozi waliohusika kwenye wizi huo ambao haujawai kutokea tangu nchi kupata Uhuru basi wao watachukua maamuzi magumu ambayo Rais huyo akuyataja maamuzi gani.

2 comments:

Anonymous said...

Hatukubaliani na kufunika swala hili la wizi mkubwa kiasi hiki, Serikali ya CCM inahusika moja kwamoja na viongozi hao wahusika wanajulikana kabisa warudishe hiyo fedha haraka na wachukuliwe hatua mara moja wakijiuzulu nyadhifa zao mara moja. Rais KIKWETE UNALAKUSEMA MOJA KWAMOJA bila hata ya kuchukua siku chache hata ukiwa huko AMERICA tunataka tukusikie unalisemeaje hili sio swala la kungoja urudi tafadhali kama unawapenda walipa kodi wako.. asante/

Anonymous said...

Rudisheni hiyo fedha na mjiuzulu haraka iwezekanavyo, NAPE hili halina ubishi na wala lisiwe la kisiasa. MBATIA UKO WAPI SIJAKUSIKIA?? ZITTO JE !!