Advertisements

Friday, December 12, 2014

BALOZI WA MAREKANI AMTEMBELEA WAZIRI CHIKAWE OFISINI KWAKE JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akimkaribisha Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress (kulia) pamoja na maofisa wa ubalozi huo, ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.Waziri Chikawe na Balozi huyo walizungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na Ofisi ya Balozi huyo nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na Ofisi ya Balozi huyo nchini. Balozi Childress alimtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana
Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake, jijini Dar es Salaam jana, kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Ubalozi wa Marekani na wizara. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments: