ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 14, 2014

CHAGUZI ZA MITAA KATIKA PICHA JIJINI DAR

Kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Mtendeni Kata ya Kisutu kama kinavyoonekana katika picha wapiga kura hawakuweza kupiga kura kutokana na kwamba na wagombea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) wa kata hiyo kukosa wapinzani na hivyo kupita bila kipingamizi,.
Mkazi wa karikoo Mashariki , Kata ya Kariakoo akipiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Lumumba ,kwa ajili ya kuchagua viongozi wa Serikali za mitaa Mitaa akiwemo Mwenyekiti na Wajumbe leo jijini Dar es Salaam.

Wakazi wa Kariakoo Mashariki, Kata ya Kariakoo wakishiriki katika upigaji kura katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Lumumba katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa leo jijini Dar es Salaama
Msimamizi wa upigaji kura, Mwalimu Lucy Buzuka akitoa maelekezo kwa wapiga kura wa Kariakoo Mashariki, Kata ya Kariakoo jinsi ya kupiga kura katika zoezi la kuchagua viongozi wa Serikali za mitaa ambapo siku ya leo jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Upigaji Kura Faudhia Mbawala akihakiki majina ya washiriki wa wapiga kura katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Hekima Buguruni, wanaongalia kutoka kushoto ni Abasi Mzee wakala wa Chama cha Mapinduzi, Omary Issa Wakala wa CUF na Abubakari Said Wakala wa ADC,leo jijini Dar es Salaam.
Wakazi wa Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala wakiwa katika foleni ya kuhakiki majina yao kwa ajili ya lupiga kura na kuweza kuwachaguwa viongozi wao wa Serikali za Mitaa katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Kimanga, leo jijini Dar es Salaam
Mkazi wa Buguruni Wilaya ya Ilala akishiriki zoezi la kupiga kura katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Hekima, kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa leo jijini Dar es Salaam.Picha na Lorietha Laurence

No comments: