Advertisements

Thursday, December 18, 2014

DKT. BILAL AMTUNUKU SHAHADA YA UZAMIVU, RAIS KIKWETE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtunuku shahada ya heshima ya Uzamivu (PhD) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete, kwa kutambua mchango wake katika Jamii, kitaifa na kimataifa pamoja na kufanikisha kuanzishwa kwa Taasisi hiyo. Dkt Jakaya alitunukiwa Shahada hiyo wakati wa Mahafali ya pili ya Taasisi hiyo yaliyofanyika leo Jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtunuku shahada ya Sayansi Uhandisi na Hesabu PhD, James Philip, wakati wa Mahafali ya 2 ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye Mahafali ya 2 ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyofanyika leo jijini Arusha.
Baadhi ya wahitimu...
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Baadhi ya wahitimu...
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake ambaye ni Mkuu wa Taasisi hiyo, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake ambaye ni Mkuu wa Taasisi hiyo, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika maandamano na viongozi wa Taasisi hiyo pamoja na wahitimu, wakati wa Mahafali ya 2 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika leo jijini Arusha. Picha na OMR

12 comments:

Anonymous said...

kazi kweli ipo hivi shahada huwa zinatunukiwa kihole holela hivi....

mwaka huu tutayaona mengi na kuyasoma mengi yetu macho tuu ha ha ha ha

Anonymous said...

Bro. usikonde. Kwa Tanzania udaktari na uprofesa si kazi kuupata! Tunao Profesa Maji Marefu, Dkt. Amour, na wengine wengi!

Anonymous said...

ha ha ha kweli kabisa kwa tanzanai kupaa udaktari na uprofesa si kazi ha ha ha profesa maji marefu ha ha ha.you made my day man for really ha ha ha

Anonymous said...

Kuna PHD za kusoma elimu na singinewe za kupewa za heshima so kuna different msikurupuke tu kuki changanya zote zakusoma.

Anonymous said...

Hawa wakuu wa vyuo Bongo wanamfanya presidenta kama mfalme JUHA

hata diamond domo pana the platinum alipewa naye phd.

angaliyeni taswiri ya wasomi wahitimu walivyo nunua na kuona wao wanasota watu wanapeana kiholela holea hizi Phd.

akimaliza utawala aenda kaamalize master yake ya economic pale UD

Anonymous said...

Wanaompa si ndio wale alio wateua. Ni kulipa fadhila. Angejua kuwa hastahili angewaambia inatosha. sasa bado UDSM, SUA, Mwalimu Nyerere, Ardhi n.k. Hawa wengine wasipompa maanake wamemdharau.

Anonymous said...

Kwa wanaojua vema chuo hicho hawatashangaa, ni chuo cha ajabu kabisa, yaani kwa kifupi ni chuo cha aibu? wanafunzi waliomaliza chuo mwaka jana mpaka leo hii hawajapewa vyeti. Maktaba hakuna vitabu, na mtandao naskia ni duni kabisa. Hebu angalia website yao harafu niambie kama ni chuo kikuu cha sayansi na technologia au kiblog cha mtu kijijini.

Wanfunzi wanasema hakuna subscription hata moja ya maana kwa international journals, na huko maabara ni aibu zadi. Hakuna reagents. Wanafunzi wanamaliza bila kukidhi vigezo, ikiwemo publication katika international journals. Naskia hilo wanafumbia macho maana wangemaliza wanafunzi si zaidi ya wanne pengine. kimekuwa chuo cha kisiasa, kuridhishana. Taifa linaangamia kwa elimu.

Anonymous said...

yaani kuna watu wana wivu wa kike,kikwete kapewa hiyo phd na wasomi kutokana na wasomi kutambua mchango wake,mlitaka iende ufipa?yaguju

Anonymous said...

Barabara ya kuelekea mandela university ni mbovu,toka moshono,chekereni hakufai.
Kikwete kapitishwa barabara ya moshi kupitia CDTI licha ya barabara kupitishwa greda majuzi

Anonymous said...

Muwe makini wakati mwingine hizi Phd huwa zinatolewa kama kejeli. We jiulize kila uchao unachanja mbuga ughaibuni kuomba omba, hospitali hakuna dawa, wanafunzi wanakosa mikopo, watu wanakwapua pesa za umma, wakati huku watu wanakufa kwa kukosa huduma hospilini wewe unakwenda kutibiwa ng'ambo, EPA, Richmond, rada na Escrow vyote hivyo ni kashfa yako halafu watu wanakupa phd na uprofesa. Ukiwaza vizuri hizo ni kejeli

Anonymous said...

Binafsi nakubaliana kabisa na Kikwete kupewa hizo degree hata kama zingekuwa 100. maana huyu ndo rais pekee aliyoinvest vya kutosha katika elimu kuliko rais mwengine yeyote yule kati ya marais wanne wa Tz.
kutoka shule za sekondari around 1500 mpaka around 10,000
kutoka vyuo vikuu chini ya 6 mpaka karibia 34
kutoka kuzalisha walimu 800 kwa mwaka hadi kufikia around 3000
ni taahira tu ambaye hawezi kuyaona haya. hata kama matokeo hatutayaona leo bila sha siku sio nyingi tutayaona.
Kikwete you deserve all those PhD.
Au nyie mlitaka afanyeje? Kupitia utawala wa kikwete hata sisi tusio wa kilimanjaro tuna shule za sekondari kwenye kata zetu. kilichobaki ni kuziimarisha tu.

Anonymous said...

Nyerere alipata Phd 23 na awards kibao, Mkapa alilamba 9 na Mzee Mwinyi alilamba PHD 8 but kati yao hakuna alojiita "Dr" or "Prof"