Jolly Tumuhirwe akiwa mahakamani leo.
Jolly Tumuhirwe alipokuwa akimtesa mtoto Arnella.
HAUSIGELI aliyenaswa kwenye video akimtesa mtoto nchini Uganda, amefikishwa mahakamani leo.
Mfanyakazi huyo Jolly Tumuhirwe ameiambia mahakama kuwa anajutilia kile alichokifanya na anaomba msamaha.
Ameshitakiwa kwa kosa la kumtesa mtoto Arnella.
Licha ya taarifa ya polisi kusema Jolly atashitakiwa kwa kosa la jaribio la mauaji, kiogozi wa mashitaka alimshitaki Jolly kwa kosa la kumtesa mtoto mdogo.
Bi.Tumuhirwe alikiri makosa yake na kuomba msamaha. Hakuna wakili yeyote aliyemwakilisha Jolly mahakamani licha ya mmoja wa mawakili mashuhuri kusema angemwakilisha Jolly bila malipo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Jumatano ambapo hakimu anatarajiwa kutoa hukumu yake dhidi ya Jolly.
Huenda akafungwa jela miaka 15 au kutozwa faini ya dola mia nne au adhabu zote mbili.
BBC


2 comments:
Mmm
Simtetei ila inawezekana nae anamatatizo ya kiakili au situation ya kazi nayo..
.1:kitu alichokifanya ni kibaya sana kinaumiza mi ni mmoja wa watu ambaye niliumia kama mzazi
2:but; hawa maboss wa kibongo nao wananyanyasa sana mahousegeli ..kama nilivyosema sitetei kabisa swala hilo la kupiga mtoto ni la kinyama na ni lazima aadhibiwe vikali ila ninaomba maboss nao waache kunyanyasa mahousegeli wao..wapeni mishahara yao mapema na walipeni vizuri..kutokana na kazi zao za ndani, nimeona hivi vitu sana maboss wanavyonyanyasa mahouse girl..inauma haswa ukiwa umebahatika kuishi hizi nchi za wenzetu ukirudi nyumbani wasaidizi wanateswa mpaka unaanza kujiuliza hivi hawa watu wanajua kwamba hata wafanyakazi wana haki zao?inategemea nini ukimuacha na hawa malaika wa mungu?watawatesa kama wewe unavyowatesa..mi naona tuwe waangarifu nabkauli na matendo yetu jinsi ya kuwafanyia watu wema..mtoto anae kusaidia kukaa na watoto wetu tuwapende ninkazi ngumu sana kulinganisha wengi wametoka familia duni..tuwasaidieni tuwapende wawe sehemu ya maisha yetu..tuwasaidie tuwapende wanahitaji kupendwa wengi ni watoto...usiwafanyie vitu ambavyo hutaki mtoto wako afanyiwe..
narudia tenabkitendo ni cha kinyama msamaha hautoshi na jela ni sehemu ya sheria lakini haitamsaidia huyu binti...tukifuatilia kiidogo u wont believe labda nae anapigwa nabkutukanwa kila siku..si make excuse ya yeye kupiga mtoto..ila nasema tuu maboss tue makini..midomo yetu na matendo yanaendana na matumaini yetu kwa watoto wetu..MUngu atusaidia amsaidie Arnella asahau...maumivu yake na aendelee na afya njema ila pia tusilipe kwa ubaya tumuombee huyo dada ..upendo ni amani
Post a Comment