ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 8, 2014

UKIFANYA HAYA, HAUSIGELI HATAKUCHUKULIA MUMEO

Ni Jumatatu nyingine tunapokutana katika uwanja wetu huu murua, tukijuzana, kuelimishana na kujadiliana kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo uhusiano wa kimapenzi. Namshukuru Jalali kwa kuniwezesha kuiona tena siku hii, naamini na wewe msomaji wangu uko poa kabisa.

Mfumo wa maisha ya familia nyingi siku hizi unawalazimu wahusika kutafuta wafanyakazi wa ndani (mahausigeli) kwa ajili ya kuwasaidia kazi. Ni uamuzi mzuri kwa sababu hurahisisha kazi ya kutunza familia na wengi huwa msaada mkubwa, achilia mbali wale wachache wenye tabia zisizofaa.

Hata hivyo, kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, vilio vya wanawake waliopo kwenye ndoa kulalamika kuibiwa waume zao na wasichana wa kazi vinazidi kuongezeka. Katika kila wanawake kumi wanaoishi na wasichana wa kazi, saba waliwahi kutendwa kwa waume zao kusaliti ndoa na mahausigeli au kujaribu kuwashawishi wavunje nao amri ya sita. Wanawake wengi ambao wapo katika uhusiano rasmi watakuwa mashahidi wa hili.

Yaani unaenda kumchukua dada wa kukusaidia kazi za nyumbani kijijini, unamleta mjini, unamhudumia kwa kila kitu, anaanza kuoga na kupendeza na mwisho unajikuta ukisaidiwa hata yale ambayo hukuomba kusaidiwa au ambayo hayastahili kuwa na msaidizi.

Wanawake wengine wanajeruhiwa zaidi baada ya waume zao kuishia kuwapa mahausigeli ujauzito au kuzaa nao! Dada wa kazi anageuka na kuwa mke mwenzio. Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili na ningependa tuzijadili kwa pamoja.

1. KUJISAHAU
Wanawake wengi wana kawaida ya kujisahau wanapopata wasichana wa kuwasaidia kazi. Kama kipindi cha nyuma kabla hajapata hausigeli mwanamke alikuwa akimfulia mumewe, kumuandalia chakula kizuri na kutunza vizuri familia, akishapata dada wa kazi, hujisahau na kuacha kutimiza wajibu wake kama mke.

Matokeo yake, unakuta dada wa kazi ndiyo anashughulikia mambo yote muhimu yanayomhusu mume kuanzia anapoamka asubuhi mpaka usiku. Ndiyo! Mumeo akiamka asubuhi, dada wa kazi ndiyo anaenda kutandika kitanda, anamuandalia maji ya kuoga, anamuandalia kifungua kinywa na kumnyooshea nguo za kuvaa siku hiyo.

GPL

3 comments:

Anonymous said...

Wanawake wenzangu hebu tusaidiane, mwanaume akishahamua kutembea nje huwezi ukafanya chochote. Hata kama unafua pika three course meals, mwogeshe wapi? Tena wewe anakuona mjinga kweli, in short nataka kuwambia just do the basic usijitese Sana. Kama anakupenda hataenda nje.

Wanawake wenzangu ,wanaume wote hataufanye nini lazima watatembea nje ,awaweze kuwa na mwanamke mmoja ,,cha muhimu labda uombe sana asipate magonjwa,maana uko nje wanachokifata .stail za ajabu.na kuchunwa,