Advertisements

Sunday, December 21, 2014

HIGH CLASS NA MKUBWA NA WANAWE WATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA

Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe Saidi Fella (kulia) akikabidhi sehemu ya misaada kwa Kituo cha Hisani.
Sehemu ya misaada iliyotolewa na High Class Look na Mkubwa na Wanawe.
Saidi Fella, wasanii wa Kundi la Mkubwa na Wanawe katika picha ya pozi baada ya kutoa misaada.
Picha ya pamoja baada ya zoezi la kutoa misaada.
Yamoto Band wakitoa burudani kidogo baada ya kukabidhi misaada hiyo.

KABLA ya kuzungumza chochote Napenda kutoa shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu kwa kila jambo ambalo limefanikiwa ni kwakupitia yeye aliye Muweza wa yote, Pili nawashukuru Watanzania wote karibu kila nyanja kwa kuonyesha ushirikiano wao kwa Mkubwa na wanawe mpaka kufikia hapa hii leo.

Mkubwa na Wanawe kwa kuungana na kampuni Mpya ambayo inajishughulisha na uuzaji na ununuaji wa vifaa mbalimbali katika mtandao High Class Look, Imeamua kutoa kidogo walichojaliwa kwa jamii kwa msimu huu wa sikuku.

High Class Look na Mkubwa na Wanawe waliweza kutembelea kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala Maji Matitu kijulikanacho kama Hisani na kutoa misaada mbambali ikiwa pamoja na vyakula na mahitaji mengine madomadogo.

Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe Saidi Fella amesema kuwa wameamua kutoa msaada huo kwani yeye pia ni yatima amepoteza wazazi wake wote wawili lakini pia pesa nyingi ambazo wanazipata kupitia show zao ni wale wale wazazi watoto hao walipo kuwa hai walikua wanahudulia matamasha yao na sivibaya leo tukiwakumbuka watoto wao.

Kwa upande mwingine Saidi Fella amewaomba watu wengine ambao wanajiweza na kuweza kutoa msaada wajitokeze kusaidia kwani bado watoto hao wanamaitaji na sisi wengine ni yatima watarajiwa.

Kwa upande wa mmiliki wa kituo hicho Bi Hidaya amesema kuwa changamoto bado ziko nyingi sana kituoni hapo, ya kwanza ikiwa nyumba kwani wamepanga na nyumba ndogo na watoto wako zaidi ya 50, lakini pia chakula na pesa karo kwa watoto wanaosoma shule

Toka ianzishwe Yamoto Band leo leo ni siku ya furaha kwetu kusheherekea Mwaka mmoja ambao umefanyika kuwa na mafaanikio mengi makubwa, moja kati ya mafanikio hayo ni kuuza kazi zetu kweye mtandao na kukuletea kokote ulipo mpaka majumbani

Nakwa hiki kidogo tulichokipata sisi ukijumuisha na furaha tuliyo nayo ya kutimiza mwaka mmoja tumeona nibora tugawane na wenzetu ambao ni wahitaji haswa kwa msimu huu wa sikukuu kama tulivyozoea kufanya toka kipindi chanyuma kwani hawa ni sehemu yetu kama wanajamii wenzetu..

na kwawale wapenzi na washabiki wa Yamoto Band tupo tayari kukupatia kilichobora zaidi endapo utahitaji kazi zetu wasiliana nasi utakuletea mpka nyumbani kwako.

2 comments:

Anonymous said...

hawa watoto hawahitaji misaada wanahitaji mama na baba wakuwalea wamekusa kitu hicho mchukuwe motto mmoja au wawili mlee kama mwanao ndo kinachohitajikia si misaada hiyo halafu hamuonekani mpaka mmsimu ujao.
waleeni kama wanenu na kuwapa faraja tena kwa kuwa na wazazi.

Anonymous said...

Annon wa hapo juu toa mfano anza wewe kuchukua mmoja wengine watafuata.