ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 30, 2014

HUNDI YA WAPONZA MISS TANZANIA

Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza alisema moja ya sababu ya kufungia mashindano hayo ni waandaaji, Kampuni ya LINO kutoa hundi feki ya malipo ya kibali ya Sh2Milioni.

BARAZA la Sanaa na Taifa (Basata) jana Jumatatu lilitoa sababu za kuyafungia mashindano ya Miss Tanzania kwa miaka miwili ikiwemo Kampuni ya LINO kuwasilisha hundi feki katika baraza hilo.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza alisema moja ya sababu ya kufungia mashindano hayo ni waandaaji, Kampuni ya LINO kutoa hundi feki ya malipo ya kibali ya Sh2Milioni.

“Walituletea hundi muda mfupi kuelekea siku ya shindano tukawaamini lakini kumbe ilikuwa feki na hadi leo leo hawajalipa,” alisema.

Mkurugenzi wa LINO, Hashimu Lundenga alisema: “Basata walichelewa kuipeleka benki hundi tuliyowapa, lakini tunakiri ilikuwa na makosa na tumekubaliana tutawalipa.
”CREDIT 
: MWANASPOTI

No comments: