Advertisements

Tuesday, December 16, 2014

MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI SAMPULI ZA MADAWATI KWA SHULE ZA MSINGI MADARASA YA AWALI LINDI MJINI

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na binti Naida Seleman anayesoma darasa la awali katika Shule ya Msingi ya Rahaleo mara baada ya Mama Salma kukabidhi sampuli za madawati aliyoyatoa kwenye Shule za Manispaa ya Lindi Mjini tarehe 15.12.2014.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akikabidhi sampuli za madawati yaliyotolewa na Taasisi ya WAMA kwa Afisaelimu wa Mkoa wa Lindi Ndugu Gift Kyando kwa ajili ya Shule za Msingi zenye madarasa ya awali katika Manispaa ya Lindi Mjini. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Shule ya Msingi ya Raha leo.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akitoa hotuba fupi kabla ya kukabidhi sampuli za madawati yaliyotolewa na Taasisi yake kwenye shule za Msingi kwa ajili ya madarasa ya awali katika Manispaa ya Lindi Mjini kwenye sherehe fupi iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi Rahaleo.
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma Madarasa ya Awali katika Shule ya Msingi ya Rahaleo wakiwa pamoja na walimu wao wakipiga makofi ikiwa ni ishara ya kumpokea Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati anawasili shuleni hapo. Picha na John Lukuwi

No comments: