Advertisements

Monday, December 15, 2014

MARCIO MAXIMO AONDOKA YANGA

Habari rasmi toka ndani ya klabu ya Yanga zinasema kuwa kocha Mbrazil Marcio Maximo ameondoka ndani ya klabu hiyo .

Habari hizi zinakuja dakika chache baada ya Millardayo.com kuripoti tetesi zinazohusu8 mustakabali wa kocha huyo Mbrazil.
Maximo anaondoka Yanga baada ya uongozi wa klabu hiyo kukubaliana naye kuvunja mkataba wake baada ya kushindwa kuelewana juu ya jinsi ya kuiendesha klabu hiyo kwenye masuala ya ufundi .

Yanga ilishikilia msimamo wa kumuajiri mkurugenzi wa ufundi ambaye alipangwa kuwa Charles Boniface Mkwasa jambo ambalo Maximo hakukubaliana nalo.

Nafasi ya Maximo sas aitachukuliwa na Mholanzi Hans Van Der Pluijm ambaye aliifundisha timu hiyo kwa nusu msimu baada ya kufukuzwa kwa Mholanzi mwenzie Ernst Brandts .

Tukio hili linaendeleza historia ya Yanga kufukuza makocha baada ya kufungwa na Simba kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe baada ya kufukuzwa kwa Ernst Brandts msimu uliopita kufuatia kipigo cha 3-1 mbele ya Simba iliyokuwa inaongozwa na Dravko logarusic.
Credit:Millard Ayo.

No comments: