Yaua mume, mke walioketi barazani, Barabara zafunikwa, Dar kizaazaa
Mvua kubwa iliyonyesha leo Jumatatu Desemba 29, 2014, kwa takriban dakika 30 katikati ya jiji la Dar es Salaam, ilitoshas kabisa kuleta mafuriko kwenye barabara kadhaa na hivyo kufanya sheeda kubwa miongoni mwa madereva, waenda kwa miguu, pikipiki na naiskeli kwani kila mahala palijaa maji. Mfano wa barabara zilizofurika maji ni hii ya PAMBA
Binti akiyaingia maji yaliyotuama kwenye eneo la katikati ya jiji jirani na kituo cha daladala Posta Mpya
Hivi ndivyo ilivyokuwa leo katikati ya jiji
Mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam na maeneo mengine nchini jana, zilisababisha maafa na kizazaa kikubwa kwa wakazi huku miundombinu mbalimbali hususan ya barabara katika mitaa mbalimbali ikifinikwa maji.
Jijini Dar es Salaam, mvua hizo zilianza saa 4:30 asubuhi na kunyesha kwa nguvu kwa takriban saa mbili, hali iliyosababisha barabara katika mitaa mbalimbali ikiwamo ya Posta na maeneo ya katikati ya jiji hilo kufurika maji na kufanya magari kupita kwa shida.
Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ulibaini kuwa maeneo mengi katika ya Jiji na mabondeni, yalifurika maji na kusababisha magari mengi na pikipiki kupita kwa shida huku na waenda kwa miguu nao wakitembea kwa taabu.
Aidha, hali hiyo ilisababisha foleni kubwa za magari katika baadhi ya mitaa hasa katikati ya Jiji.
Hata hivyo, hakukuwa na taarifa zozote za vifo katika Jiji la Dar es Salaam kutokana na mvua hizo licha ya kuwapo kwa usumbufu mkubwa kwa wakazi wake.
MUME, MKE WAFA WAKIWA BARAZANI
Wakati hayo yakitokea jijini Dar es Salaam,
mkoani Tabora watu wawili, mke na mume, wakazi wa kijiji cha Lughubu kata ya Itumba wilayani Igunga, wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba yao kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani humo.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 11:00 jioni wakiwa wamekaa barazani kwenye nyumba wanayoimiliki wanandoa hao, Ernest Makala (90) na mkewe Pelepetua Petro (80).
Akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga, mmoja wa watoto wa marehemu, Anastazia Ernest, alisema wazazi wake walikuwa wamejipumzisha nyumbani kwao, lakini ghafla ukuta wa nyumba ulibomoka na kuwaangukia walipokuwa wamekaa.
“Ni kweli sisi watoto tumepata pigo kubwa kwani wazazi wetu wawili wamefariki dunia, mimi nilipigiwa simu na majirani wakiniambia wazazi wangu wamepondwa na ukuta wa nyumba. Nilipofika katika eneo la tukio, nilikuta baba amefariki dunia," alisema Anastazia huku akibubujikwa na machozi.
Mtendaji wa kijiji cha Lughubu, Hussein Mohamed, alisema yeye baada ya kufika eneo hilo, alikuta wananchi wakiwa tayari wametoa kifusi cha udongo wa nyumba iliyoanguka huku mume, Ernest Makala, akiwa tayari amekwisha kufariki dunia.
“Mimi nilikuta tayari mwanaume akiwa amefariki dunia na mkewe alikuwa mahututi," alisema mtendaji huyo wa kijiji.
Alifafanua kuwa kutokana na hali aliyokuwanayo Pelepetua, wananchi waliamua kumkimbiza katika Kituo kidogo cha Afya kilichopo kata ya Itumba kwa matibabu, lakini Mganga wa kituo hicho, Efulay Malima, aliwashauri wampeleke Hospitali ya Wilaya ya Igunga.
Hata hivyo, alisema walipofika hospitali, Pelepetua alifariki dunia kabla ya kupewa matibabu.
Kaimu Mtendaji wa Kata ya Itumba, Twalib Ngahoma, aliwataka wananchi wa kata hiyo kuwa makini kwa kipindi hiki cha mvua za masika kwa kuchukua tahadhari mapema ikiwamo kutokaa karibu na nyumba zenye nyufa ikiwa ni pamoja na kukaa mbali na miti iliyopo karibu na nyumba zao.
Aidha, mtendaji huyo alisema mbali ya vifo hivyo, pia nyumba 25 ikiwamo ya marehemu hao, zilianguka kutokana na mvua hiyo iliyonyesha siku tatu mfululizo.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Sono Nyaga, alithibitisha kufariki dunia kwa watu hao na kuongeza kuwa vifo hivyo vilisababishwa na kuangukiwa na kuta za nyumba waliyokuwa wakiishi.
HALI YA HEWA WATOA TAHADHARI
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), ilisema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha kwa sasa ni za kawaida na zitaendelea kwa siku tatu mfululizo.
Akizungumza na NIPASHE jana, Mkurugenzi wa TMA, Dk. Agness Kijazi, alisema mvua za msimu wa vuli zimechelewa kwani zilipaswa kuanza Oktoba hadi Desemba, mwaka huu.
Alisema mvua zilizoanza kunyesha jana jijini Dar es Salaam na kwingineko nchini, zimechelewa kutokana na Pwani ya Somalia kuwa na ongezeko la joto na upepo usio na unyevu nyevu kuvuma kuelekea ukanda wa Tanzania, hivyo kuwa na joto badala ya mvua huku kukiwa na mkandamizo mdogo wa hewa kwa upande wa Msumbiji.
“Ni hali ya kawaida ndani ya msimu wa mvua kuwa na uwezekano wa mvua kubwa…mvua hii itaendelea kwa siku ya kesho (leo) na Desemba 31, mwaka huu, ikipungua au kuongezeka kwa kiwango tofauti,” alisema.
Aidha, aliwataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kuwa uwezekano wa mvua kuwa kubwa upo, na kwamba inaweza kuleta madhara.
Dk. Kijazi pia aliwataka wananchi kufuatilia kwa karibu taarifa mbalimbali zinazotolewa na vyombo vya habari kuhusu utabiri wa hali ya hewa wa kila siku

CHANZO: NIPASHE
2 comments:
VIVA ZE MIUNDOMBINU & THE MINISTERI OF UJENZI!!
viva ufisadi na mafisadi wote wa nchii hii.
chukueni chenu na mapema wananchi wafe na mfuu.
Post a Comment