Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela.
Watu watatu wamefariki dunia na wengine 11 kujeruhiwa vibaya katika matukio mawili yaliyozua taharuki kwa wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.
Katika tukio la kwanza lililohusisha ajali ya gari dogo aina ya Toyota Noah likitokea Tanga kwenda Moshi Mjini, liliacha njia na kupinduka baada ya dereva wake, Ally Kasim (48) kushindwa kulimudu kutokana na mwendo kasi.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 10:45 jioni katika barabara kuu ya Same-Mwanga na kuwataja waliokufa kuwa ni Batuli Mhina (55) na Amina Alli (7) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Mchepuo wa Kiingereza ya Majengo, mjini Moshi na wengine kumi kujeruhiwa.
Miili ya watu hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa ya KCMC huku majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.
Katika tukio la pili, Elion Mtui (49), mkazi wa Kijiji cha Masiha, Wilaya ya Moshi, amejinyonga kwa kutumia nguo maarufu kama mtandio kutokana na ugomvi wa kugombea fedha kati yake na mkewe, ShoseMungu Elion (47).
Kamwela alisema chanzo cha kifo hicho ni baada Sh. 200, 000 zilizotumwa na binti yao, Jesca Elion kupitia M-pesa ya namba ya simu ya mama yake, hivyo kutokea kutokulewana kuhusu mgao wa fedha hizo.
Muda mfupi baada ya kuzuka ugomvi huo, marehemu Elion alimshambulia mwilini mkewe katika sehemu mbali mbali na kumjeruhi vibaya, tukio liliwalazimu majirani kumkimbiza katika Hospitali ya Kitemboni-Marangu na mumewe kuamua kujinyonga.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment