ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 16, 2014

MWANASHERIA MKUU AJIUZULU

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.

5 comments:

Anicetus said...

Mtu wa kawaida akiiba embe Kariakoo anapigwa mawe; viongozi wakiiba wanachafua hewa

Anonymous said...

one down..

Anonymous said...

Hii yote ni chezea toto...dangany'a toto hapa. JK usichezee akili za watanzania. Watanzania wa LEO si wa JANA!
Asante

Anonymous said...

Kwa kweli aibu ilioje ku-jaribu kujustify kwamba walichofanya hawa Jamaa ni uchafuzi wa hali ya hewa tu. It is despicable utter shameful for JK and all the culprits.

Anonymous said...

We Werema rudiaha pesa za watanzania la sivyo hatuchkui mawe tutaonana na COM kwenye box la kura. Huwezi kuishi tanzania kama uko mbinguni wakati watanzania wengine hawajui mlo unaofuata wataupataje