ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 16, 2014

RAIS DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI ZA MSIBA WA MAMA MZAZI WA KULWA,DOTTO NA NICO MWAIBALE, MWILI WASAFIRISHWA KWENDA MBEYA LEO KWA MAZISHI.

 
 Kulia ni Kulwa na kushoto ni Dotto Mwaibale wakiwa na sura za Majonzi wakati wa Ibada fupi ya Kumuombea Mama yao Mpendwa kabla ya kuanza Safari ya kwenda Mbeya
Wa kwanza Kulia ni Mdogo wao wa Mwisho wa Akina Mwaibale Ambwene  na wa pili kutoka kulia ni Dada yao Mkubwa wa akina Mwaibale  Mary Anyitike ambaye ni Kamishna Mkuu Msaidizi wa Skauti  Shughuli za Vijana Taifa
 
 Mwili wa Marehemu Bi. Twitikege Mlagha Mfumu
mama yao Dotto, Kulwa na Nico Mwaibale ukiwa unaandaliwa tayari kwa kuombewa, Kuagwa na kusafirishwa
 Mchungaji Ephraim Mwakajwanga Akiwa anaongoza Ibada ya Kumuaga Mama mzazi wa Dotto, Kulwa na Nico Mwaibale  Bi. Twitikege Mlagha Mfumu leo katika Hospitali ya Temeke
 Baba Mchungaji akitoa Neno la Kiroho (Mahubiri mafupi) wakati wa kuuaga Mwili wa Marehemu, Katika Mahubiri hayo alisisitiza kuwa Duniani tunapita kila kitu kinabaki hivyo ni vizuri kila mmoja ajiandae  na kuwa mama ametangulia na sisi tunafuata hivyo yatupasa kuwa tayari
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers Abdalah Mrisho akitoa salam za Rambi rambi kwa wafiwa ambapo Kulwa Mwaibale anafanyia kazi hapo.
Joachim Mushi akisoma utaratibu na kutoa maelezo mbalimbali wakati wa shughuli za kuuaga mwili wa Marehemu.
 Muwakilishi kutoka Jambo Concept ambao ndio wachapishaji wa Gazeti la Jambo leo ambapo Dotto Mwaibale anafanyia kazi huko Mkurugenzi Beny Kisaka wakitoa salam za Rambi rambi ambapo walitoa mkono wa pole wa kiasi cha Shilingi Laki tano.
 Muwakilishi kutoka Skauti ambako Dada yao Mkubwa wa akina Mwaibale anafanyia kazi akitoa salam za Rambi rambi
 Msemaji wa kwa Niaba ya Familia Noah Mwakalasya  akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya wanafamilia na kushukuru kwa moyo waliojitolea kuja kumsindikiza mama yao mpendwa
Dada Mkubwa wa akina Mwaibale  Mary Anyitike ambaye ni Kamishna Mkuu Msaidizi  wa Skauti Shughuli za Vijana Taifa akisoma wasifu wa Marehemu mama yao
 Baba Mchungaji akitoa Neno la Mbaraka wakati wa kumaliza ibada ya kumuombea Marehemu Mama yao Kulwa, Dotto na Nico Mwaibale kabla ya kuanza safari kuelekea Mbeya kwa Mazishi.
 Mdogo wa Mwisho wa akina Mwaibale Ambwene  akitoa salam za Mwisho kwa Marehemu mama yake
 Dada Mkubwa wa akina Mwaibale Mary Anyitike ambaye ni Kamishna Mkuu Msaidizi  wa Skauti Shughuli za Vijana Taifa akitoa salam za Mwisho za kuuaga mwili wa Marehemu Mama yao
 Dotto Mwaibale Akiaga Mwili wa Marehemu mama yake
Kulwa na Dotto Mwaibale wakiuaga Mwili wa Marehemu mama yao
 Kulwa Mwaibale akiwa ameshikiriwa na ndugu zake Baada ya Kuaga Mwili wa Mama yake
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers Eric Shigongo akiwa anaaga Mwili wa Marehemu
 Muhidin Issa Michuzi Mmiliki wa Michuzi Blog akitoa Heshima za mwisho katika Mwili wa Marehemu
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers Akitoa Heshima za Mwisho katika Mwili wa Marehemu
Muhidin Issa Michuzi wa katikati na Abdalah Mrisho wa kwanza kulia wakimpa pole Dotto Mwaibale
Kulwa na Dotto Mwaibale wakiwa katika ya pamoja na Baadhi ya waandishi kutoka Jambo leo, Global Publishers, Habari Maelezo na vyombo vyengine vya Habari
Baadhi ya Bloggers wakiwa katika Msiba wa Mama yao Dotto, Kulwa na Nico Mwaibale kutoka kushoto ni Geoffrey Adroph  wa Pamoja Blog, Cathbert Kajuna wa Habari na Matukio Blog na Joachim Mushi wa The Habari blog
Baadhi ya  Waombolezaji wakiwa katika Majonzi
 
Waombolezaji wakiwa katika Shughuli ya Kuuaga mwili wa Mama yao Dotto,Kulwa na Nico Mwaibale 


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atuma salamu za Rambirambi katika Familia ya Mwaibale Kwa kuondokewa na Mama  Mzazi wao mpendwa Bi.Twitikege Mlagha Mafumu aliye fariki majira ya saa 5 usiku siku ya jumamosi wakati akikimbizwa hosipitali ya hindra kwaajiri ya Matibabu

Akiwasilisha salaamu hizo kwaniaba ya Rais Jakaya Kikwete Meneja Mkuu wa Globabal Publishers Limited Abdalah Mrisho Ameweza  kutoa pole  kwa wafiwa wote kwa ujumla wakiwakilishwa na Kulwa,Dotto na Nico Mwaibale Hivyo Kuwa na Moyo wa uvumilivu katika kipindi kigumu kilicho wafika familia ya Mwaibale

Vilevile Aliweza simama Kwa niaba ya Wanahabari Abdalah Mrisho aliweza kufikisha salaamu hizo Kwa kuwapa pole familia na wote walio guswa na msiba wakiwemo ndugu,jamaa na marafiki wa ndugu yetu mpendwa ambaye kwa sasa ni marehemu Bi. Twitikege Mlagha Mafumu

Mwili wa ndugu yetu Mpendwa  umeagwa leo Mchana majira ya saa 6 katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke na kuanza safari  ya kuusafirisha kwa kwenda  kumpumzisha  mama mpendwa katika kijiji cha Kibumbe,Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya  ambapo Anatarajiwa kuzikwa  kesho Tar 17 alasil mwezi wa kumi na mbili (12) Mwaka huu

Tunapenda kutoa pole kwa wafiwa wote na Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema peponi 
Amen

No comments: