Sunday, December 7, 2014

RAIS KIKWETE ATEUA MKUU MPYA MMOJA WA MKOA NA KUWAHAMISHA VITUO VYA KAZI WENGINE SITA

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mkuu Mpya mmoja wa Mkoa na kuwahamisha vituo vya kazi wengine sita kuanzia jana, Jumamosi, Desemba 6, 2014.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumapili, Desemba 7, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Rais amemteua Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha, Ndugu Daudi Felix Ntibenda  kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Ndugu Ntibenda ataapishwa kesho, Jumatatu, Desemba 8, 2014, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar Es Salaam.
Taarifa hiyo inasema kuwa wakuu waliohamishwa vituo vya kazi ni Mheshimiwa Elaston Mbwilo anayehamishwa kutoka Mkoa wa Manyara kwenda Mkoa wa Simiyu ambako anachukua nafasi ya Mheshimiwa Paschal Mabiti aliyepewa likizo ya ugonjwa, Mheshimiwa Joel Nkanga Bendera aliyehamishwa Mkoa wa Manyara kutoka Mkoa wa Morogoro na Mheshimiwa Dkt. Rajabu M Rutengwe anayehamishwa Mkoa wa Morogoro kutoka Mkoa wa Tanga.
Wengine ni Mheshimiwa Magalula Saidi Magalula anayehamishiwa Mkoa wa Tanga kutoka Mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza anayehamishiwa Mkoa wa Lindi kutoka Mkoa wa Pwani na Mheshimiwa Mhandisi Evarist B. Ndiliko anayehamishiwa Mkoa wa Pwani kutoka Mkoa wa Arusha.
Wakuu wengine wa mikoa wanaendelea kubakia katika vituo vyao vya sasa vya kazi.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

6  Desemba,2014

2 comments:

Anonymous said...

Wakuu wa mkoa kuhamisha kunasaidia nini..badala kusafisha weziwa ESCROW hata kuongelea haongelei kama halioni ..hasifanye watu watoto wadogo hapa aanze kujiangalia yeye mwenyewe na waziri wake wizi tuu na kudanganya danganya wananchi aacha mheshimiwa rais kama utasoma hii komenti ni kwamba tumechoka na kudanganywa kila siku

Anonymous said...

Kabisaa ..hapo umeongea manakebmpaka leo Tanzania kuna watu hawana maisha kabisa, yaani hawajui dunia inaendaje mheshimiwa kila siku wee nje ya nchi...tunaelewa wee ni rahisi..lakini sasa wizi nyumbani mbona unaangali nimetoka tanzania nyumbani sakata zima ni kero..escrow escrow hata kulizungumzia na utakaa kimya litaisha hivi hivi ..mtazamo nini kwa nchi? Mheshimiwa raisi wee ulikuja marekani ukaanza kuponda kutwa tunashindwa kwenye mablogs..hatuachi mablogs kwa sababu mnaumiza roho sana .familia zenu zinaishi vizuri..hizo pesa mnazoiba nakufunikiana kwa nini msisaidie kidogo , hamjisikii vibaya jamani watu shida sana Tanzania maji, umeme, mpangilio mbaya wa barabara, ajali ambazo zote zinatokana nabmfumo mbovu wa pesa ..wizi na tamaa mmezidi na maneno mengi kuishi kiutemitemi acheni..mnahamisha wakuu wa mikoa ..maskini wezi wanakaa kimya inawezekana na wewe kama kiongozi unalijua hilim.waziri na wengine wawajibishe usiwakalie kimya..nyue hela mnazo zinawatosha jamani saidieni mama na bibi zetu vijijinibmsiibe sana inauma sana...