THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mkuu Mpya mmoja
wa Mkoa na kuwahamisha vituo vya kazi wengine sita kuanzia jana, Jumamosi,
Desemba 6, 2014.
Taarifa iliyotolewa
leo, Jumapili, Desemba 7, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni
Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Rais amemteua Mkuu wa Wilaya ya Karatu,
Mkoa wa Arusha, Ndugu Daudi Felix Ntibenda
kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Ndugu Ntibenda
ataapishwa kesho, Jumatatu, Desemba 8, 2014, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar Es
Salaam.
Taarifa hiyo inasema
kuwa wakuu waliohamishwa vituo vya kazi ni Mheshimiwa Elaston Mbwilo
anayehamishwa kutoka Mkoa wa Manyara kwenda Mkoa wa Simiyu ambako anachukua
nafasi ya Mheshimiwa Paschal Mabiti aliyepewa likizo ya ugonjwa, Mheshimiwa
Joel Nkanga Bendera aliyehamishwa Mkoa wa Manyara kutoka Mkoa wa Morogoro na
Mheshimiwa Dkt. Rajabu M Rutengwe anayehamishwa Mkoa wa Morogoro kutoka Mkoa wa
Tanga.
Wengine ni Mheshimiwa
Magalula Saidi Magalula anayehamishiwa Mkoa wa Tanga kutoka Mkoa wa Lindi,
Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza anayehamishiwa Mkoa wa Lindi kutoka Mkoa wa
Pwani na Mheshimiwa Mhandisi Evarist B. Ndiliko anayehamishiwa Mkoa wa Pwani
kutoka Mkoa wa Arusha.
Wakuu wengine wa
mikoa wanaendelea kubakia katika vituo vyao vya sasa vya kazi.
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es
Salaam.
6
Desemba,2014
2 comments:
Wakuu wa mkoa kuhamisha kunasaidia nini..badala kusafisha weziwa ESCROW hata kuongelea haongelei kama halioni ..hasifanye watu watoto wadogo hapa aanze kujiangalia yeye mwenyewe na waziri wake wizi tuu na kudanganya danganya wananchi aacha mheshimiwa rais kama utasoma hii komenti ni kwamba tumechoka na kudanganywa kila siku
Kabisaa ..hapo umeongea manakebmpaka leo Tanzania kuna watu hawana maisha kabisa, yaani hawajui dunia inaendaje mheshimiwa kila siku wee nje ya nchi...tunaelewa wee ni rahisi..lakini sasa wizi nyumbani mbona unaangali nimetoka tanzania nyumbani sakata zima ni kero..escrow escrow hata kulizungumzia na utakaa kimya litaisha hivi hivi ..mtazamo nini kwa nchi? Mheshimiwa raisi wee ulikuja marekani ukaanza kuponda kutwa tunashindwa kwenye mablogs..hatuachi mablogs kwa sababu mnaumiza roho sana .familia zenu zinaishi vizuri..hizo pesa mnazoiba nakufunikiana kwa nini msisaidie kidogo , hamjisikii vibaya jamani watu shida sana Tanzania maji, umeme, mpangilio mbaya wa barabara, ajali ambazo zote zinatokana nabmfumo mbovu wa pesa ..wizi na tamaa mmezidi na maneno mengi kuishi kiutemitemi acheni..mnahamisha wakuu wa mikoa ..maskini wezi wanakaa kimya inawezekana na wewe kama kiongozi unalijua hilim.waziri na wengine wawajibishe usiwakalie kimya..nyue hela mnazo zinawatosha jamani saidieni mama na bibi zetu vijijinibmsiibe sana inauma sana...
Post a Comment