Profesa Tibaijuka alivuliwa uwaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Rais Jakaya Kikwete juzi kutokana na kuhusika kupokea fedha katika akaunti binafsi.
Muleba. Siku moja baada ya kufukuzwa uwaziri, Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka amewasili jimboni kwake na kusema, “Bwana alitoa na Bwana ametwaa.”
Profesa Tibaijuka alivuliwa uwaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Rais Jakaya Kikwete juzi kutokana na kuhusika kupokea fedha katika akaunti binafsi.
Baada ya kuwasili na kupokewa kwa maandamano, Profesa Tibaijuka aliwaomba wananchi kukaa kimya kwa dakika moja ili kumkumbuka katibu wake wa jimbo aliyefariki dunia wakati sakata hilo likijadiliwa bungeni.
Profesa Tibaijuka aliyepokewa kwa msafara wa magari kutoka Uwanja wa Ndege wa Bukoba, aliwaeleza wananchi kuwa ilikuwa ni lazima kutafuta msaada kwa watu wengi ili aweze kuwasomesha watoto anaowasaidia kielimu.
“Kuna suala la escrow, zamani kulikuwa na aspro ambayo ilikuwa ni dawa ya kweli, sasa suala hili limefikia tamati hamkunichagua ili nikawe waziri, ni sawa na kusema Bwana alitoa na Bwana ametwaa,” alisema Profesa Tibaijuka.
Aliambatana na mtoto wa kike akisema ni mmoja wapo wa wanafunzi wasio na uwezo anaowasomesha katika Shule ya Babro Johanson, inayotajwa kuwa ndiyo iliyopokea Sh1.6 bilioni alizoingiziwa katika akaunti yake binafsi, katika Benki ya Mkombozi.
Profesa Tibaijuka alitumia muda mfupi kuelezea suala la kuhusishwa katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow akisema Taifa lina changamoto ya kupata elimu bora na wapo viongozi wachache kama yeye wenye moyo wa kusaidia masuala ya elimu.
“Teknolojia sasa imekua, naamini mlikuwa mnafuatilia mambo yalivyokuwa yanakwenda, yalikuwa ni mambo makubwa, kazi ya uwaziri nisingeipata bila nyinyi wananchi. Nilikuwa na majukumu mengi, sasa nitapata muda wa kukaa jimboni.
“Taifa bado lina changamoto ya kupata elimu bora, hiyo shule mnayoisikia ada yake kwa mwaka ni zaidi ya Sh4 milioni, hivyo lazima nitafute mtu wa kunisaidia. Hakuna mtoto wangu hata mmoja anayesoma kwenye shule hizo,” alisema Tibaijuka.
Huku hotuba yake ikikatizwa na watu waliokuwa wakishangilia, Profesa Tibaijuka aliwaonya wanaotaka kulinyemelea jimbo hilo kuwa yuko ‘fiti’ na anawasubiri kukutana nao ulingoni.
Alisema atakuwa tayari kufanya kazi katika maeneo yanayoongozwa na vyama vya upinzani jimboni kwake akiamini kuwa pia wapo wanachama wa CCM.
Credit:Mwananchi.

4 comments:
Wewe mama usimuingize Mungu kwenye mambo yako mabaya na ubabe wako, nenda Muleba ukale matoke halafu rudi Dar upumzike kwenye hekalu lako halafu rudisha pesa za wananchi. Tena una bahati sana kama ungekuwa NYC ungekuwa RIKERS ISLAND kwa miaka 10 na mwanao angekuja kukutembelea. Kumbuka maneno ya marehemu mzee Kalinjuma.
Ni mijizi tu kazi ya kungàngània madaraka ili muibe pesa za wananchi yaani hamuoni aibu wala haya?wakati huduma za wananchi zinahitajika!Nampongeza Rais kwa kufanya uamuzi mzuri kwa kuwang`oa madarakani, na wengine wezi wote wafuate kungòlewa madaraka pia.Viongozi hamjapewa madaraka kusubiri kula pesa za wananchi,Mmepewa madaraka muchape kazi na mnalipwa mishahara yenu na marupurupu kibao kwani hizo haziwatoshi?
I wonder huyu mama aliwezaje ku-run wizara ingali kashindwa kumlea mtoto wake vema.Binti ni kushinda kumwaga mitusi mitandaooni...ustaarabu zero.
Huyu Prof ni mjinga sana amepokea "ETI MCHANGO WA SHULE" then she deposited to her personal bank account that school doesn't have bank account to day to day operations? or you're getting ready to buy presidency next year? Sorry for underestimate Tanzania that nobody will know your dirty game. if your bro gave u a gift you should deposited it to school's account u will be a minister now, JK deserve to fire u and u don't deserve to represent anybody if you fail in simple logic like that
Post a Comment