Wiki iliyopita tulianza kuijadili mada ya kama kuna umuhimu wowote wa kumuandalia mwenzi wako fumanizi endapo ukihisi au ukigundua kuwa anakusaliti kwa kutoka nje ya ndoa?
MAONI YAKO YAKOJE?
Nilipoitambulisha mada hii, niliomba tushirikishane mawazo kwani mimi si mjuaji wa kila kitu. Nikushukuru wewe uliyeshiriki kwa kutoa maoni yako kupitia ujumbe mfupi wa maneno (SMS). Natamani kila ujumbe ulionifikia niuchapishe lakini nafasi inanibana. Zifuatazo ni baadhi ya meseji:
1. UNATAFUTA SABABU YA KUACHANA
Haina haja ya kumwandalia fumanizi mwenzi wako kwani kwa kufanya hivyo ni kujenga chuki baina yako na mpenzi wako labda kama humpendi na unatafuta njia ya kuachana naye unaweza kufanya hivyo ili upate kigezo ila kama unampenda usifanye hivyo. Bad Ksoo, Tandika.
2. NILIZIMIA SAA TATU NILIPOFUMANIA
Unapopanga kufumania inabidi ujiandae kwanza kisaikolojia. Mimi niliwahi kumfuma mpenzi wangu tena akivunja amri ya sita na rafiki yangu kipenzi na nilipanga fumanizi ili kuhakikisha kama ninachoambiwa ni kweli.
Nilikuwa siamini kwa jinsi tulivyokuwa tunaishi akionesha kunipenda sana. Hatimaye fumanizi likafanikiwa, siku hiyo mimi nilishindwa kufanya uamuzi, nilizimia saa tatu, dah! Inauma sana. Willy Mwakasanga, Temeke.
3. NI AIBU KUBWA SANA
Kwanza niseme ni fedheha kubwa kumuandalia mwenzi wako fumanizi. Iweje uandae kwa kuwataarifu hata ambao walikuwa hawajui mchepuko wa mkeo/mumeo? Pia ni aibu kubwa kwa wanao na wataathirika sana kisaikolojia, hata wakiwa shuleni watakosa raha kwa kuchekwa na wenzao.
Nyamong’ang’ana Kekarambwe, Geita.
3. NI AIBU KUBWA SANA
Kwanza niseme ni fedheha kubwa kumuandalia mwenzi wako fumanizi. Iweje uandae kwa kuwataarifu hata ambao walikuwa hawajui mchepuko wa mkeo/mumeo? Pia ni aibu kubwa kwa wanao na wataathirika sana kisaikolojia, hata wakiwa shuleni watakosa raha kwa kuchekwa na wenzao.
Nyamong’ang’ana Kekarambwe, Geita.
4. FUMANIZI NDIYO DAWA YA MSALITI
Katika kuandaa fumanizi mimi naona kuna umuhimu ili utakapoona au kugundua utakuwa na ushahidi kwamba uliyenaye si mkweli na hana nia njema na wewe maana moyo wa binadamu hauna macho ila akili ndiyo hukataza na kuchanganua zuri na baya.
Utakapogundua ukweli sidhani kama moyo wako utaendelea kumpenda tena katika siku za uhai wako na ni vizuri kufuatilia nyendo za mtu wako ili ujue kama upo sahihi kumpenda au la! Shaibu, Kigamboni.
5. FUMANIZI NI UDHALILISHAJI
Hakuna umuhimu wa kumwandalia fumanizi mkeo, mumeo au mpenzi wako wakati bado unampenda. Kwa mke au mume mwenye busara hawezi kumdhalilisha mwenzi wake, ni aibu kwako wewe uliyefanya hivyo. Nampenda mpenzi wangu na ikitokea nikahisi kitu kibaya kwake, nitakaa naye na kumwambia.
Josephine Maembe, Tabata Kisiwani, Dar.
HITIMISHO
Hakuna tukio baya kama pale unapogundua mwenzi wako anakusaliti lakini hakuna kitu kibaya zaidi kama kumfumania.
Wataalam wa saikolojia wanashauri kwamba kama hujajiandaa kisaikolojia, hutakiwi kuandaa fumanizi. Kama unao ushahidi wa kutosha na unadhani huwezi kuendelea kuishi naye tena kwa sababu ya tabia zake za usaliti, unaweza kutumia njia za busara kukatisha uhusiano wenu.
Pia kama bado unampenda lakini unajua anakusaliti na ushahidi unao, unaweza kuzungumza naye kwa upole, ukishindwa washirikishe watu anaowaheshimu na kama kweli anakupenda, hataendelea kukusaliti, atabadilisha tabia na kutulia na wewe.
Mwisho kabisa ni kwa wale wasiotosheka na mpenzi mmoja na kuendekeza michepuko. Siku hizi kuna maradhi mengi ukiwemo Ukimwi.
Michepuko siyo ujanja, baki njia kuu na huyo mmoja uliyemchagua na kuwa mwaminifu kwake. Sote tukisimamia uaminifu kwenye mapenzi, hakutakuwa na mafumanizi wala maumivu ya moyo!
Nakutakia heri ya mwaka mpya 2015.
GPL
No comments:
Post a Comment