Wabunge wa Somali wameng'oa waziri mkuu wa taifa hilo Abdiweli Sheikh Ahmed mamlakani.
Ni mara ya nne kwamba kura ya kutokuwa na imani dhidi yake ilipigwa baada ya majaribio ya awali kumalizika kwa ghasia.
Waandishi wanasema kuwa serikali ilikuwa imelemazwa na uhasama baina ya kiongozi huyo na rais wa taifa hilo Hassan Sheikh Mohamud.
Wanasema kuwa usalama ulikuwa umezorotoa kutokana na hali hiyo.
Abdiweli ni waziri mkuu wa pili kuwahi kuondolewa madarakani mwaka huu.
Marekani imeshtumu kura hiyo ikisema kuwa haikuzingatia maslahi ya raia wa Somali.
1 comment:
ASANTE je WaTanzania mpo hapo!! kula hela wamekula, waziri mkuu ameminya! Wabunge wote mmeshindwa kumtoa kwa kura ya kutokuwa na imani ya uongozi wake! mmewaachia wezi kuendelea kuwepo madarakani na kuendelea kutumia hizo fedha kwa nini ??
Post a Comment