Watoto wenye Albinism, wakipata "msosi", wakati wa hafla ya chakula cha mchana kila mwaka inayoandaliwa na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi, kwa watu wenye ulemavu. Hafla ya mwaka huu ilifanyika pale ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, siku ya Jumapili Januari 25, 2015. Kwa uchache watu 4,000 walihudhuria hafla hiyo.
MWENYEKITI Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi, Jumapili Januari 26, 2015, kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, aliwaalika watu wenye ulemavu kiasi cha 4,000 kwenye hafla ya kila mwaka ya chakula cha mchana.
Dkt. Mengi alishiki kula nao chakula cha mchana ikiwa ni pamoja na kuwahudumia kwa kuwagawia vyakula baadhi yao.
Kama ilivyo ada, wageni wake hao walikula, walikunywa na kucheza muziki, ambapo wasanii mbalimbali mashuhuri hapa nchini wa muziki wa kizazi kipya yaani BONGO Flava, walitumbuiza.
Jambo jipya lililojitokeza kwenye hafla ya mwka huu, Dkt. Mengi aliwatangazia “Bingo” watu wenye ulemavu kote nchini, kuwa ataanzisha shindano la wazo bora la shughulki ya kibiashara itakayomkomboa mtu mwenye ulemavu, ambapo atatenga shilingi milioni 10 kila mwezi kwa washindi kumi kujinyakulia shilingi milioni 1 kama mtaji wa kunzia shughuli iliyopendekezwa kama wazo.
Hali kadhalika, hafla ya mwaka huu imekuja na neema kwa watu wenye ulemavu wa viungo, ambapo kampuni ya Kamal Steels imeahidi kutoa miguu bandia 200 kila mwaka kuwasaidia watu wenye ulemavu wa viungo kote nchini, na kwa kuanzia kwenye hafla hiyo palitolewa miguu hiyo bandia 200.
Picha kwa hisani ya K-VIS Blog
4 comments:
Nice one baba...
Mungu akubariki sana Bw. Mengi.
Huo ndio utu haswa, hongera Mr Mengi.
kampeni ya uchaguzi mapema mchana kweupeeeeeeeeeeeeeeee.
Post a Comment