Advertisements

Monday, January 26, 2015

HAKUNA SHULE, KAZI WALA NDEGE KURUKA NEW YORK ZAIDI YA NDEGE 6,000 CANCELS HADI JUMATANO

Hapa ni Times Square New York kimya kabisa wakati siyo kawaida yake tishio la barafu
inayoendelea kushuka kama imeagizwa vile yasababisha shule kufungwa hadi jumatano kazi na usafiri wa chini na anga stop kwa siku mbili.
New York ni nyumbani kwa vikwangua anga lakini kama unavyoona ni ukungu mzito na barafu ikinyesha.
 Dada akiwahi nyumbani kabla akujawa kubaya zaidi watu wameambiwa kukaa ndani na kuchoma mahindi nje ni shida
Hapa ni Penn station Kituo kikubwa cha train za kuelekea nje ya New York na miji ya jirani kama unavyoona watu wameganda kusubiri hatma za safari zao.
Kulia anatamani lakini machozi hayawezi kutoka maana yameganda na baridi ni bora ajikwinyate  na mizigo yake juu ya viti vya uwanja wa ndege  baada ya kuambiwa kuwa ndege kuruka ni majaliwa hadi jumatano.
Hapa ni uwanja wa ndege wa LaGuardia New York barafu ni hatari hata ndege uwezi kuiona mother nature ni shida ndege zaidi ya 6,000 hakuna kuruka wala kutua.
Kila mtu alikuwa na style yake ya kusikitika kutoka na hali hiyo ya kusimamishwa safari zote za ndege kiwanjani hapa.

No comments: