ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 26, 2015

NGASSA ATOWEKA YANGA FIGISU FIGISU ZIMETONYA KUWA KAENDA SAUZ

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa, ametoroka nchini na kukimbilia kusikojulikana huku viongozi wake wakijua kuwa amekwenda Tanga kwa ajili ya msiba wa mamamkwe wake.


Ngassa hajaonekana Yanga tangu Jumanne ya wiki iliyopita. Aliwaaga viongozi wa klabu hiyo kuwa anakwenda Tanga kuhudhuria msiba lakini taarifa zinadai ametoroka nchini.

Chanzo chetu cha habari kimesema winga huyo ameonekana akipanda ndege kuelekea Afrika Kusini.

Bado haijawekwa wazi kuwa amekwenda kufanya nini lakini inaaminika amekwenda katika Klabu ya Free State ya Afrika Kusini kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.
Championi Jumatatu ilipomuuliza katibu wa klabu hiyo, Dk Jonas Tiboroha, alisema Ngassa aliwaaga kuwa anakwenda msibani Tanga ambapo alifiwa na mamamkwe na si vinginevyo.

“Sisi alituaga kuwa alipatwa na matatizo ya kifamilia, kwamba alifiwa na aliondokewa na mamamkwe wake, kama ni hizo habari nyingine binafsi sina,” alisema Dk Tiboroha.

Chanzo cha habari chetu kilikwenda mbali na kusema kuwa, uongozi hautaki kuliweka wazi suala hilo ingawa wameandaa adhabu ya kutosha kama fundisho kwa wachezaji wengine kwa ukosefu wa maadili ya kikazi.

“Kuna watu walimuona akipanda ndege ya Sauz, kwa hiyo viongozi wanasema bado wanalichunguza kwa umakini ili wajiridhishe kuhusu safari yake na iwapo itabainika kweli alikuwa Sauz, kitakachomkuta ni siri yao, ila ni adhabu ambayo itakuwa fundisho kwa wenzake wanaofanya mambo ya Kiswahili,” kilisema chanzo chetu.

Ngassa alipotafutwa kwa simu yake ya mkononi ambayo amekuwa akiitumia Tanzania, hakuweza kupatikana kwa siku nzima ya jana, hali inayoonyesha kuwa hayupo nchini.

Kwa siku za hivi karibuni, Ngassa amekuwa katika mgogoro wa chinichini ya Yanga, hasa kutokana na uongozi wa klabu hiyo kukiuka makubaliano ya kumlipia kiasi cha Sh milioni 45 anachodaiwa na Simba kutokana na adhabu aliyopewa na TFF kwa kusaini klabu mbili mwaka 2013.

Yanga ilikuwa imekubaliana na kiungo huyo kwamba itamlipia nusu ya deni wakati alipokuwa akisaini kuichezea Yanga mwaka 2013 na kiasi kingine watakuwa wakimkata kidogokidogo kwenye mshahara lakini badala ya kumkata Sh 500,000 kama makubaliano yalivyo, wamekuwa wakimkata Sh 1,000,000 hali inayodaiwa kumuondolea morali na kumfanya acheze chini ya kiwango.

1 comment:

Anonymous said...

asepe akisanzuwe akitoa huko alikokendana atokomea toka alivyoweka ule mkanda wake wa ngono na mdogo wa mwinjilisti moja hapa dar maarufu (jina sitosema) nimejenga chuki sana naye,yani mwanamme gani anamdhalilisha mwanamke kwenye mitandaoni.kweli unajua kupenda?

wakina dada muwangaliye sana wanaume walio maarufu wenye majina; wenye kutajika na wenye pesa msivifuate vitu hivi sana najua maisha magumu sana but mwisho wa siku mtakuja kuwekwa mitandaoni na sijui wapi mtaficha nyuso zenu.atatamani kufa na siku zenu bado. mtataka kujiuwa na mtatenda dhambi kwa muumba wenu.

ni ushauri tu wabure.

luca naomba weke hii comment please kwa sababu natoa tahadhari tu kwa wakina dada zetu,maana si mila na tamaduni zetu kuwekwa kwenye mitandaoni bila kupenda mwenyewe wakati wa tendo la ndoa.

tahadharini sana wakina dada zangu.bora kupendwa na maskini na anaye kuthamini na kukupenda kikweli kuliko kufanywa chombo cha burudani bila wewe kujijua.