Advertisements

Sunday, January 25, 2015

Lungu ashinda uchaguzi wa urais Zambia

Edga lungu kulia aliyeshinda uchaguzi wa urasi nchini Zambia

Mgombea wa chama cha Patriotic Front Edga Lungu ameshinda uchaguzi wa urais nchini Zambia.

Tume ya uchaguzi nchini humo imesema kuwa Lungu amepata asilimia 48 ya kura zilizopigwa.

Alikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa upinzani Hakainde Hichilema.Raia wa zambia wakati wa kampeni za ucvhaguzi wa urais

Wote walikuwa wameahidi kuboresha mifumo ya elimu na kubuni nafasi za ajira.

Uchaguzi huo uliandaliwa kufuatia kifo cha rais Michael Sata ambaye aliaga dunia mwezi Oktoba mwaka uliopita. BBC

No comments: