ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 4, 2015

MWANAFUNZI AFUNGWA JELA KWA KUMTUKANA RAIS KWENYE MTANDAONI

Mwanafunzi mmoja nchini Kenya amepewa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kumtukana rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika mtandao.
Alan Wadiu Okengo mwenye umri wa miaka 25 pia atalipa faini ya dola 2,200 la sivyo ahudumie kifungo chengine cha mwaka mmoja.
Alikuwa ameshtakiwa kwa kutoa matamshi ya chuki baada ya kusema kuwa watu wa kabila la rais la kikuyu wanafaa kuwekewa mipaka katika maeneo fulani.


Mwanablogu mashuhuri nchini humo pia alishtakiwa baada ya kumwita rais Uhuru Kenyatta 'rais ambaye hajakomaa'.


Kenya ina mitandao mahiri na mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza amesema kuwa kesi hiyo imezua mjadala mkubwa kuhusu kile kilichosahihi katika mitandao

4 comments:

Anonymous said...

jina wanaomtukana raisi wetu inakuwaje na yeye awachukuliye hatua kama hii ya rais Kenyatta. shukuruni mungu sana raisi wetu mstaarabu sana na sio dictator.eti anaitwa anacheka cheka ovyoo na dhaifu,mnahitaji kutafutiwa raisi kama huyu kenyata na aliyepita Enzi zile mnazikumbuka za kupanga foleni kilo mmoja ya sukari,mchele etc ukikutwa na sabuni ya lifeboy ya kunukia unakamwata utajieleza polisi umeitoa wapi.

maraisi kama hao ndo wanaotakiwa.

Anonymous said...

Wewe anon hapo juu, hujui unachoongea kwani ukiona kitu afanyacho rais dikteta wa Kenya ni lazima na sisi tuige? Mbona hatuigi mazuri yanayofanywa na Kenya badala yake unataka tuige anayoyapenda huyo dictator Kenyatta na wenzake. Huyo rais usimlinganishe na rais yeyote wa Tanzania ....kwanza huyo ni mshtakiwa wa the Hague, sisi hatuna rais aliye mshtakiwa wa the hague. Kwanini usitulinganishe na nchi zenye demokrasia inayoeleweka? Kwa hiyo watakachofanya Kenya na hapa kwetu lazima kifanyike?

Anonymous said...

raisi wetu hajashitakiwa the hague kwa vile ni raisi handsome boy na mcheke mcheka tu,nchi yote imeshachukuliwa na watu wa nje najuta lakini atafanyaje so hawezi kushtakiwa yeye the hague huyu raisi wa Kenya ni kidume aliwakomalia kichwa ile mbaya marekani ndo maana wakamuundia njama sisi tukifanya hivyo na sisi tutashitakiwa the hague pia.

wewe ndo unaonge usichokijua unaropoka ropoka ovyoo eti nchi za kidemokrasia unadhani zipo hizo.

nenda kafunguwe tv yako na kibia chako upoze koo.huna unachokijua wewe usijifanya mjuaji sana kumbe juha.

soma alama za nyakati za kisiasa ulimwingu mzima na jinsi economic inavyokwenda za dunia nzima hasa hasa mataifa makubwa kwenda kuwameza mataifa madogo halafu njoo uje hapa tukufundishe usifoke foke sana ukajifanya wakujua kumbe juha.

Anonymous said...

rais wetu hawezi kushtakiwa the hague kwa sababu ni puppet wao kila wanachokitaka nchini kwetu wanakichukua.

unajua kigamboni kuna base ya kijeshi ya nchi yao.

unajua vitalu vya tanzanie na almasi na dhahabu sasa ni vyao.

unajua tanesco sasa umeme watatupa wao pesa zote na rasilia mali zote zinakwenda kwao sasa kwanini wamshitaki raisi wetu the HAGUE wakati hatuna ubavu wakupigana nao wala kuwakatalia.

raisi wa Kenya ndo kidume aliwakomalia kichwa. jiulize kwa nini Tanzania ilibaguliwa katika community ya east Africa wakati Uganda Rwanda na walikuwa na mikutono yao wametuona hatufai sisi ni ma puppet tu.

twendeni tukaserebuke na ngoma za diamond na nyama choma na vimwana tuwakumbatiye na tukatike katika kama madada and that is it.


hatuna uzalendo wowote ule wala uchungu na nchi yetu.

mwafyuuuuuuuuuuuuuuuu. what a shame.

vijana taifa la kesho leo wanapotea kwa unga wa sembe,na ngono kila mahali wajanja wanachukua rasilimali zetu.

halafu unatuleta hapa raisi wetu haja shitakiwa the Hague. mwafyuuuu what a shame. go and do your homework my man wacha uvivu wakutofikiria kwa sana ulimwingu wa leo.

hongera sana kenyata wache wakushitaki popote pale duniani.