ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 26, 2015

MWANAMKE AFANYA UNYAMA WA KUTISHA TABORA

Zuhura Masoud (25), akiwa kwenye karandinga la polisi nyumbani kwake mtaa wa Chamchem mkoani Tabora, baada ya kutiwa mbaroni na polisi wakimtuhumu kufanya mauaji ya watoto wake wawili wa kuwazaa na kisha kuwafukia mmoja sebuleni na mwingine chumbani kwake

MWANAMKE mmoja mjini Tabora, amewaua kwa amewanyonga watoto wake wawili wa kuzaa kisha kuwazika ndani ya nyumba.

Polisi mjini Tabora imethibitisha leo Jumatatu Januari 26, 2015, kuwa mwnadada Zuhura Masoud mwenye umri wa miaka 25, alitekeleza mauaji hayo nyumbani kwake, mtaa wa Chemchem, majira ya saa moja jioni, Jumapili Januari 25, 2015, na sasa anashikiwa na polisi kuhusiana na tukio hilo.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Tabora, Juma Bwire, aliwataja marehemu kuwa ni Mwamvua Mrisho mwenye umri wa miaka 4 na kichanga, Sudi Mrisho mwenye umri wa miezi 4.

Akielezea mazingira ya tukio hilo, Kamanda Bwire alisema, baada ya kuwanyonga wanawe, akiwatia kwenye viroba kila mmoja na cha kwake, na mmoja alimzika kwenye sebule ya nyumba hiyo na mwingine chumbani kwake. 

Polisi inawashikilia mwanamke huyo pamoja na mwanamume mmoja, aliyetajwa kwa jina la Shaban Ramadhan mwenye umri wa miaka 75, ili kuisaidia polisi kupata ushahidi zaidi wa nini kilichosababisha mwanamama huyo kuchukua uamuzi mzito kiasi hicho.

Polisi inasema, inawashikilia watu hao kwa vile, kabla ya kutokea tukio hilo, palizuka ugomvi wa kugombea nyumba kati ya mwanamume huyo anayetajwa kuwa ni baba wa mwanamke Zuhura na Zuhura mwenyewe

K-VIS Blog

No comments: