ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 26, 2015

Ni kweli Mwana FA na Diamond haziivi kisa Alikiba? FA aueleza ukweli

Weekend hii kwenye show ya uzinduzi wa Tigo Music iliyofanyika Leaders Club jijini Dar es Salaam, kulienea taarifa kutoka kwa mmoja wa mameneja wa Diamond Platnumz kuwa Alikiba aliwazuia Mwana FA na Shaa kusaliamiana na hitmaker huyo wa ‘Ntampata Wapi’.

Ni kweli?
“Sijui nikwambie nini, lakini kama sitaki kulifanya hili suala liwe habari, kiukweli yaani,” FA ameiambia Bongo5.

Vipi kuhusu uhusiano wake na Diamond baada ya kumshirikisha Alikiba kwenye hit single yake, Kiboko Yangu?

“No we are very good as a matter of fact,! amesema Binamu.

“He texts me (Diamond) every now and then, hivyo namcheck nini. Mameneja wake wote watatu washkaji zangu kinoma na yeye tuna mazoea ya kutosha tu hivi tumekaa one of these days tukapiga story sana, hakuna chochote kilichoharibika,” ameongeza rapper huyo.

“I don’t even think Kiba anamind hiyo na anajua kuwa mimi na Diamond we cool na watu wa Diamond pia we cool, they are cool with me na as a matter of fact wananitaniaga ‘wewe team Kiba wewe’. So we good like that.”

No comments: