Viongozi: Wageni rasmi wa sherehe za Muungano Mhe: Mwigulu Nchemba (wapili kulia) akifuatiwa na Balozi Mulamula, pamoja na Balozi wa Waziri wa Nchi Zanzibar, Ofisi ya Rais na MBM Dr. Mwinyihaji Makame, (wakwanza kulia) Balozi Mwinyi (kulia)Viwe Juma,wapili kulia ambae ni Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Zanzibar Heroes Abuu Qullatein katika Sherehe za Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Jijini Washington DC. Wasimamizi wa timu ya Zanzibar Heroes Seif Ameir na Dedie Rouba wakionyesha jezi walizodhaminiwa na (PBZ) Benki ya Watu wa Zanzibar.
Viongozi: Wageni rasmi wa sherehe za Muungano Balozi Mulamula(kulia) pamoja na Balozi wa Waziri wa Nchi Zanzibar, Ofisi ya Rais na MBM Dr. Mwinyihaji Makame (wapili kushoto) Balozi Mwinyi, (kushoto) wakikabidhi kombe kwa makepteni wa timu ya Kilimanjaro na Zanzibar Hero
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn Iddi Sandaly akikabidhi jezi kwa nahodha wa Kilimanjaro Seif Ndossa
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Amour, akizungumza machache kuhusu kazi na utendaji wa kazi za Benki hiyo ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na malengo yake wakati wa hafla hiyo ya futari iliyofanyika Aug 8, 2012 katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Benki ya Watu ya Zanzibar PBZ imekubali kudhamini mpambano wa mwaka huu katika sherehe ya muungano kati ya timu ya Kilimanjaro na Zanzibar Heroes za ughaibuni mechi itakayochezewa DMV katika kilele cha kuhitimisha sherehe za Muungano zinazofanyika kila mwaka DMV na kuwa sherehe zinazotambulika kitaifa na nchi ya Marekani.
PBZ wameahidi kudhamini Jezi za timu zote ikiwemo gharama za uwanja wa mechi hio inayosubiliwa kwa hamu na mashabiki wakiwemo wachezaji wenyewe ambao mwaka jana kulikuwa na upinzani mkali kutoka pande zote mbili.
Afisa Suleiman Saleh ambaye kwa sasa yupo Tanzania kwa ajili ya kutafuta wasanii watakao nogesha siku ya sherehe ya Muungano ambayo mwaka huu itakuwa ya kihistoria . Afisa huyo alipoongea na Vijimambo amesema ameishaanza kuongea na mwasanii mbalimbali akiwemo Steve Nyerere, Ali Kiba na baadhi ya wasanii kutoka Zanzibar ni Sabah Salum Mchacho.
1 comment:
muescrow hela za kiwanja tena mtupeleke mchangani.
Post a Comment