Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (mwenye koti la suti) akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Pemba kwa ajili kuhuduria sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni, Kusini Pemba na kupokelewa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph (kulia) aliyeambatana na Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu (aliyeongoza mbele).
Munekano wa sehemu ya jengo la Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba kabla ya kuzinduliwa rasmi.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyeambatana na mkewe akisalimiana na Ofisa mdhani kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar na Mjumbe wa bodi ya usimamizi Redio Jamii Micheweni, Ali Mohamed mara baada ya kuwasili eneo la tukio.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph wakipitia ratiba kabla ya kuanza rasmi sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani uliofanyika Kusini Pemba.
Mke wa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bi. Fainula Kurji-Rodriguez (kushoto) na Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu wakifurahia burudani ya Ngoma ya Msembwe ya Kusini Pemba ilipokuwa ikisherehesha kabla ya kuwasili wa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.
Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akijumuika kutoa burudani na kikundi cha Ngoma ya Msembwe kutoka Kusini Pemba.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (ZBC), Chande Omar (kulia) akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) kabla ya kuanza kwa sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani iliyopo Kusini Pemba. Katikati ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph na kushoto ni Mke wa Mratibu Mkazi wa UN Tanzania, Bi. Fainula Kurji-Rodriguez.
Meneja wa Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni Mkoani Kusini Pemba, Bw. Ali Abbas akisoma risala ya kituo chake mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto visiwani Zanzibar, Mh. Zainabu Omari Mohammed (hayupo pichani) wakati wa sherehe za uzinduzi wa kituo hicho cha redio.
Mabinti wa visiwani Pemba wakisoma utenzi wa kulishukuru shirika la UNESCO na ZBC kwa kuanzisha kituo hicho cha Redio jamii jimbo la Mkanyageni mkoani Kusini Pemba.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo visiwani Zanzibar, Juma Yakufi akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri mwenye dhamani ya wizara hiyo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni mkoani Kusini Pemba uliofanyika mwishoni mwa wiki visiwani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba, Hemedi Selemani akitoa neno la shukrani wakazi wa mkoani jimbo la Mkanyageni pamoja na wageni waalikwa kwenye sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani ya Kusini Pemba uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza kwenye uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani ya Kusini Pemba uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimkabidhi cheti Meneja wa Redio Jamii Mkoani ya Kusini Pemba, Bw. Ali Abbas wakati wa sherehe za uzinduzi wa Redio jamii hiyo.
Meza kuu.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba, Bi. Mwanajuma Abdallah akizungumza machache na wakazi wa mkoani na kuwaasa kukitumia chombo hicho vyema katika kujiletea maendeleo na kupashana habari kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua rasmi kituo hicho cha Redio Jamii.
Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed akisoma hotuba yake kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo cha redio ya jamii jimbo la Mkanyageni, Mkoani Kusini Pemba.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wakazi wa Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi kwenye sherehe za ufunguzi wa kituo hicho cha Redio Jamii.
Pichani juu na chini ni Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed akikabidhi vyeti kwa baadhi ya wafanyakazi wa Redio Jamii Mkoani ya jimbo la Mkanyageni mkoani Kusini Pemba. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo visiwani Zanzibar, Juma Yakufi.
Mgeni rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha Redio Jamii Mkoani iliyopo Kusini Pemba. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba, Bi. Mwanajuma Abdallah (mwenye mtandio wa bluu), Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba, Hemedi Selemani pamoja na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Sasa kimezinduliwa rasmi....!
Mgeni rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed akitia saini kitabu cha wageni cha kituo cha Redio Jamii Mkoani Kusini Pemba kabla ya kukagua vifaa na studio ya kituo hicho.
Mgeni rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed akizungumza Live na wananchi wa jimbo la Mkanyageni mkoani Kusini Pemba mara baada ya kuzindua kituo cha Redio Jamii Mkoani ikiwa ni shamra shamra ya sherehe za Mapinduzi mwishoni mwa wiki kisiwani Pemba. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na washika dau kutoka UNESCO.
Mtangazaji wa kituo cha Redio Jamii Mkoani ya Kusini Pemba, Bw. Seif Mohammed akiwa kwenye mahojiano na Mgeni rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed yaliyorushwa Live na kituo hicho mara baada ya kuzinduliwa.
Mgeni rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Redio Jamii Mkoani, Wajumbe wa Bodi ya Redio Jamii Mkoani, wafadhili pamoja na baadhi ya wageni waalikwa.
Mgeni rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba.
Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akiwa kwenye picha na wanafunzi wake wa vituo vya redio jamii ya Mkoani na Micheweni mara baada ya sherehe za uzinduzi.
Kikundi cha Ngoma ya Msembwe cha kisiwani Pemba kikitoa burudani kwenye uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani uliofanyika mwishoni mwa juma Kusini Pemba.
Na Mwandishi wetu, Pemba
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema kwamba itaendelea kuruhusu kuanzishwa kwa Redio za jamii kutokana na umuhimu wake katika kuhimiza maendeleo na kutumika kama daraja kati ya wananchi na serikali yao.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Zainab Omar Mohammed wakati akizundua kituo cha redio ya jamii jimbo la Mkanyageni, Mkoani Pemba.
Shughuli hiyo ambayo ilifanyika kama sehemu ya shamra shamra za sherehe za mapinduzi kutimiza miaka 51 zilihudhuriwa pia na wafadhili wa mradi huo ambao ni Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Waziri huyo alisema kwamba uzinduzi wa kituo cha redio ya jamii katika jimbo la Mkanyageni Mkoani Pemba ni moja ya azma ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwapa haki wananchi wake ya kupata habari ikiwa ni sehemu muhimu sana ya maisha ya wanadamu.
Alisema habari ni kitu muhimu sana katika maisha ya sasa na wakati taifa likiadhimisha miaka 51 ya mapinduzi yaliyolenga kubadili maisha ya wazanzibari uwapo wa redio za jamii ni kitu ambacho kitasukuma mbele zaidi madhumuni ya mapinduzi , kumkomboa mzanzibari kiuchumi na kifikira.
“Redio hizi Jamii, zimewekwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa madhumuni ya kuwapa fursa wananchi kupata habari,kupata burudani, kupata elimu, lakini pia kutoa fursa ya kutoa mawazo yao kupitia redio hizi ili serikali ipate kujua zaidi nini hasa changamoto za wananchi na iweze kuzifanyia kazi kwa urahisi zaidi” alisema Waziri Zainab.
Pamoja na kuushukuru Umoja wa mataifa kwa kusaidia redio za jamii aliutaka Umoja huo uendelee kuimarisha uwezo wa redio hizo ili wananchi wazitumie kupata maendeleo.
Naye Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amesema Umoja wa mataifa unajisikia fahari kuwezesha asilimia 60 ya wazanzibari kusikiliza redio za jamii na kuzitumia katika maendeleo yao.
Alisema umoja huo utaendelea na ushirikiano wake na serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya kuweka mazingira ya upatikanaji wa habari kuwa bora zaidi, ushirikiano ambao waliuanza mwaka 2008 wakati wa kutengeneza sera ya utangazaji.
Alisema ni sera hiyo iliyowezesha kuwepo kwa redio za jamii na utangazaji wa umma.
Alisema Redio za jamii ni msaada mkubwa katika kutoa elimu kwa jamii inayozunguka kituo hicho na kusema kwamba ni imani yake kituo cha Mkoani kitafanya kazi iliyokusudiwa kwa kuhamasisha mawazo chanya ya maendeleo na kuleta ushirikiano na amani inayotakiwa katika jamii.
Amesema Umoja wa Mataifa umewezesha kituo hicho vifaa vya utangazaji na kutengeneza uwezo wa wafanyakazi wa chombo hicho.
Amesema kupitia mradi wa uwezeshaji demokrasia (EDP) unaoendeshwa kwa pamoja na UNESCO na UNDP chini ya makubaliano ya msaada kwa serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa (UNDAP) , Umoja wa Mataifa umetoa mtambo wa kurushia matangazo wenye nguvu za Watts 600 unaoweza kusambaza matangazo yake eneo lote la Kusini pemba.
Pamoja na mtambo huo na vifaa vingine vya studio vilitolewa na kumefanyika ufundishaji wa watangazaji namna bora ya mawasiliano na menejimenti ya habari na utawala.
Mratibu huyo aliitaka serikali na taasisi zake kukitumia vyema kituo hicho katika kuhakikisha kwamba maendeleo yaliyokusudiwa kwa jamii yanapatikana kupitia vipindi mbalimbali vya kuelimishana.
Pia aliwataka waendeshaji wa kituo hicho kuwa makini na kuwajibika kwa umma, kauli ambayo awali pia ilielezwa na Naibu Katibu Mkuu , Wizara ya habari Utamaduni , Utalii na Michezo Juma Yakufi aliyetaka sheria na taratibu za mawasiliano kuzingatiwa.
Alitaka vipindi vitakavyotengenezwa kuzingatia utu, silka na utamaduni wa Mzanzibari na redio hiyo kuendeshwa kwa mujibu wa masharti ya redio jamii kwa kuhakikisha hawaingiliwi na taasisi yoyote na kuendeshwa kwa manufaa ya jamii na sio manufaa ya mtu mmoja mmoja.
Naye Mwa redio hiyo Ali Abbas pamoja na kushukuru kusaidia kuanzishwa kwa redio hiyo aliitaka jamii kuitumia vyema nafasi waliyopewa kuendeleza mbele maendeleo yao na kutumia upashanaji habari kutanzua changamoto za maendeleo.
No comments:
Post a Comment