ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 25, 2015

SHILOLE AWAPA MAKAVU WANAOMTUKANA

SHILOLE AWAPA MAKAMU WANAOMTUKANA
Katika hali isiyokuwa ya kawaidi msanii shilole amefunguka na kutoa ya moyoni kuhusu mashabiki wanao wa-follow wasanii katika mitandao ya kijamii kutokana na baadhi ya mashabiki kutumia mitandao hiyo kuwachafua wasanii hao kutokana na kuwakejeli hadi kufikia hatua ya kuwatukana hadharani kupitia mitandao hiyo.Kupitia A/C yake ya Instagram shilole ameposti ujumbe huu kuhusu baadhi ya mashabiki wenye tabia ya kuwakashifu wasanii kupitia mitandao hiyo.
“Hivi mashabiki zangu niwaulize swali!?? Hivi unapom-follow mtu ili uwe unamtukana TuuĆ¹u kila akipost picha yake?? Au unam-follow ili upate kuona anafanya nini?? Katika kazi , kiukweli mimi nakelekwa sana na baadhi ya mashabiki zangu naona kama wakuwa sio wazalendo kabisaaĆ  kila ufanyalo yeye kwake anaona baya tu acheni roho za kwanini! Ukiona mtu kafanya vizuri msifie tu na kama unaona hajakufurahisha mwambie tu kwa uzuri kwani matusi hayajengi! “
Shilole aliendelea;
“Mimi kama msanii nategemea maoni yenu mazuri na sio matusi yenu tujaribu kuiga mifano kwa nchi za wenzetu wanapenda wasanii wao na kuwajali lakin huku sisi kutwa mnatuchamba loh! Na sisi pia wakati mwingine tunaumia na matusi yenu yasio na maana! But ukitaka kunitukna uwe na tusi jipya la 2015 yani unitukane huku unanipa PESA. Nawapenda sana team support wasanii wa home kuweni na J2 njema”-

2 comments:

Anonymous said...

shilole ,shish baby ha ha ha umenifurahisa kweli kwa kusema tuwe na tusi jipa la mwaka mpya tunakutukana na tunakupa PESA Ha ha ha ha nimependa sana hii.uko juu mummy.

na nikweli mkifanya mema tuwasifiyeni na si kuutukaneni kila siku,umesema kweli mummy.

but anayekutukana pia angalia si wote wana nia mbaya sometime bora yule anayekutukana kuliko anayekusifu sifu kila leo kila kukicha ujua hakutakia mema anaye weza kukutukana basi ujue huyo ndo rafiki anakutakia pia mema sema kwa wakati ule utaona matusi tu yake.

rafiki na mpenzi na fan wako wa kweli akikutukana yapima matusi hayo utaona kuna kaukweli au roho ya kwanini.

anayekupenda kweli lazima atakupa pia machungu na makavu asiyekupenda atakuramba miguu yako huku ukimpa kisogoa ANAKUNGONGAAA. ANGALIA SANA WATU KAMA HAWA SHILOLE SHISH BABY.

Mdau kwa baba Obama ndani ya mjengo mweupe.

your truly biggest fan na ukikosea anakukosoa. na ukifanya vema anakusifiaaaaaaaaa weeee mwisho wa maelezoooooooo.

Anonymous said...

Sasa dada Shish baby ukisoma maoni ya watu ilhali ukiwa kioo cha jamii utaweza kuishi kweli? Lol..ushauri wa bure wasanii wenzako hawasomi maoni hususan kama huna roho ngumu kaa mbali na maoni ya watu. .kazi zako unauza ndiyo cha msingi inatosha huna haja ya kupekua na anasema nini..kama ni kuumia basi muulize Diamond atakupatia ushauri.