ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 26, 2015

Siri ya Muhongo yafichuka, Wafanyabiashara, wawekezaji wakubwa wahusishwa

*Yaelezwa wivu, majungu,fitina chanzo kingine
*Wabaya wa Muhongo sasa wajipanga kufanya sherehe
Said Mwishehe
SIKU moja tu baada ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kuamua kuachia ngazi katika wizara hiyo siri kubwa imefichuka ya sababu hasa ambayo imemfanya aondoke ukiachilia mbali sakata la Escrow.

Imebainika kuwa wizara hiyo ni ngumu kwa waziri kukaa muda mrefu kutokana na kile kinachoelezwa kuwa wafanyabiashara na wawawekezaji wakubwa na wadogo wamekuwa wakitumia mbinu chafu kuhakikisha mambo yao yanafanikiwa na wanapoona kuna kikwazo lazima waziri husika aondolewe.

Akizungumza kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini mmoja wa wanasiasa mahiri nchini, aliliambia Jambo Leo kuwa, Prof.Muhongo ameondoka katika wizara hiyo si kwasababu ya Escrow ila majungu na fitna za kisiasa zimechangia kwa sehemu kubwa.

Alisema kuwa Wizara ya Nishati na Madini imekuwa ni tamanio la wafanyabiashara na wawekezaji wa kada mbalimbali na kwa mazingira hayo wamekuwa na mbinu chafu za kufanikisha mambo yao.

“Unapokuwa waziri mzalendo na unayetanguliza maslahi ya Taifa unaonekana mbaya mbele ya wafanyabiashara na wawekezaji wenye mbinu chafu za kibiashara,”alisema mwanasiasa huyo.

Alisema hata mawaziri ambao wamekaa muda mrefu katika wizara hiyo hakuna ambaye alikuwa anafurahia wizara hiyo maana imekuwa na majungu mengi hasa ya kisiasa na hizo mbinu chafu za wafanyabiashara wakubwa ndani na nje ya nchi.

“Kwa msimamo wa Prof.Muhongo katika kusimamia maslahi ya umma, ndio maana amefanyiwa kila aina ya mbinu chafu za kumuondoa.

“Hili sakata la Escrow kwa Muhongo hakuwa anahusika nalo lakini nguvu ya majungu na fitna za wanasiasa hawa wabunge ndio zimefanya afikie uamuzi wa kuachia ngazi,”alisema.

Alitaja baadhi ya mawaziri waliopita katika wizara hiyo katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete ni Waziri wa Nishati na Madini, Ibrahim Msabaha, Naziri Karamagi, Wiliiam Ngeleja na Prof.Muhongo na sasa George Simbachawene.

Hata hivyo, Ngeleja ndiyo aliyekaa kwa muda mrefu ambapo yeye amekaa kwa nafasi ya Naibu Waziri mwaka mmoja na kisha Waziri wa Nishati na Madini kwa miaka minne na nusu ambapo kwa ujumla amekaa miaka mitano na nusu.

Wakati Karamagi alikaa kwa muda wa mwaka mmoja na nusu,Msabaha alikaa katika wizara hiyo kwa miezi sita na Prof.Muhongo amekaa kwa miaka miwili na nusu na Simbachawene yeye atakaa kwa muda wa miezi nane.

“Ni vigumu kudumu kwa muda mrefu katika wizara hiyo.Imejaa maneno mengi na wakati huo huo maadui wanakuwa wengi, kila ambaye anamahitaji yake yasipofanikiwa lazima aendeshe kampeni ya kukuondoa.

“Hili la Escrow limekuwa kama chanzo tu la wenye malengo mabaya kwa taifa kutumia mwanya huo kuhakikisha Muhongo anaondoka na hata ingekuwa si hilo la Escrow angetafutiwa namna nyingi ya kumuondoa.Ndivyo palivyo pale,”alisema mwanasiasa huyo.

Mbali ya kubainika kwa sababu iliyofanya Muhongo kuamua kuachia ngazi, taarifa nyingine zinaeleza kuwa, wabaya wa Prof.Muhongo ambaye walikuwa wakipambana usiku na mchana kuhakikisha anaondoka katika wizara hiyo wanajiandaa kufanya sherehe ya kujipongeza kwa madai kuwa wameshinda mapambano dhidi yake.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika ni kwamba, wabaya hao wa Prof.Muhongo wameanza mkakati wa kuhakikisha wanakutana na kufanya sherehe hiyo ambapo imeelezwa inatarajia kufanyika mwishoni mwa wiki hii.

Wakati hayo yakiendelea, Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila, ametoa msimamo wake kuwa, Prof.Muhongo mbali ya kujiuzulu hatua ambayo sasa inatakiwa kuchukuliwa na Serikali ni mpeleka mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Kafulila alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, ambapo alisema kujiuzulu pekee haitoshi kwani fedha ambazo zimepotea ni nyingi ambazo zingesaidia kuleta maendeleo kwa nchi lakini zimeliwa na wajanja wachache.

JAMBO LEO

12 comments:

Anonymous said...

Uongozi ni dhamana na kwa bahati mbaya au makusudi kabisa tunashindwa kufahamu miiko ya uongozi. .mtu leo masikini kesho akipewa nafasi ya uongozi anabadilika tena ghafla tu anakuwa tajiri...Muhongo amewekewa pesa na billion na mfanyabishara. .kwa kiongozi makini anefahamu miiko ya uongozi asingechelewa kurudisha alichopokea na serikali makini ingeshamfikisha mahakamani..haihitaji akili nyingi kutenganisha zawadi ya pesa na uongozi ...lakini kwa bongo hata Rais anashindwa kutambua hilo!! Hivi muuza njugu na Rugemalila nani anaweza kukaribishwa kwenye ofisi ya Muhongo? Ifike mahali turekebishe sheria na tuwe wakali kwa viongozi wachafu! Kama hunielewi basi safari ya maendeleo bongo daima itabaki kuwa ndoto tena ya mchana .

Anonymous said...

Good point msemaji hapo juu. Nchi inaliwa utafikiri hakuna kesho. Hivi wakijiuzulu ndiyo mwisho wa sakata? Kumbe ukiwa leader, ukila hela zaq umma adhabu ni kujiuzulu. Abekuwa mtu wa kawaida angefungwq 30 years. Majaji nao wanapokea rushwa, how rotten is the system.

Anonymous said...

Mdau hapo juu una ushahidi gani kwamba Muhungo kapewa billion na mfanyabiashara? Tueleweshane kwa sababu taarifa zote rasmi hazionyeshi kwamba Muhongo ni miongoni mwa wale walioshikishwa na Rugemarila.

Anonymous said...

Wadau wawili wa kwanza hawakusoma huu waraka. Wametoa maoni yao tu kwa jazba.

Anonymous said...

Prof. Muhogo is one of the few leaders educated and worked abroad for 30 yrs. He went back home to help lead the country in the proper direction, unfortunately if you don't take rushwa, you abide by the rules, you stop rich Business men from getting richer, you are not going to survive in Tanzania. Ask everyone at wizara ya nishati, they can testify that. Few hungry powerful business men who want to continue to run their business illegally by bribing the Ministers pushed him out because he didn't take any bull shit from them. It's really sad to see a good leader going out like that.

Anonymous said...

If you are in Rome do as the romans do!! Pole Professor.

Anonymous said...

Nakubaliana na mdau wa hapo juu. Ndiyo maana wasomi wengi tumekimbilia ughaibuni, tunaitwa "Brain Drains"... I am proud to be one of them! Wacha tuwaachie nchi hao wenye mashahada ya Political Science , History, na Kiswahili waangushe nchi! Labda siku moja JWTZ litaamuka na kuwanyosha hao wanasisa. Prof. Muhongo, jumuika nasi ughaibuni, utapata ridhiki tele na kuutumia ujuzi wako.

Anonymous said...

muhogo katolewa naye kafara kama tibainyuka three more to go, mmoja top leader na anayumfuata msaidizi wake na mwingie wewe chini ya msadizi wake tunawasubiri wajiwajibishe wenyewe.

si alishema ardhi itachimbika akilazimishwa kujiuzuru sasa imekuwaje?

serikali yote ya ccm iko corrupts hakuna hata mmoja asiyechukuwa rushwa na kutoa rushwa wameingia madaraka kwa rushwa na wameifanya TANZANIA KAMA SHAMBA LA BIBI

ISITULETA BLA BLA BLA ZENU HAPA.Hakuna cha muhongo wala kiaazi hapa.

WOTE UKOO WA PANYA NA NDO MAANA WENGINEWE WAMEGEUKA KUWA MAPANYA BUKUUUUUUUUUUUUUU.

aliyekuwa msafi peke yake alikuwa hayati moringe sokoine.angekuwepo leo hii mafisadi wenge koma na kushika adabu zao.

sokoine alikuwa hapendi mtu mtawala ajifanye mungu mtu alishasema akikosea mkuu yeyote lazima akosolewe asiabudiwe kama mungu.

mungu amlaze mahali pema kwa kweli tuna kumiss sana baba Edward moringe sokoine.

Anonymous said...

like his name muhongo, muongoooooooo.

Anonymous said...

Wasomi wamethibitisha kuwa sio waaminifu hata kidogo Tanzania. .siasa za kusema eti msomi atatukomboa zilishapitwa na wakati..unaweza kuwa na degree 10 lakini uongozi ni kipaji na uaminifu hauletwi na degrees ni utu wa mtu..Mnamtetea kwa kuwa ni msomi? Ebo!!! Kwani Tibaijuka si msomi? Acheni ulimbukeni uliopitwa na wakati..

Anonymous said...

ukoo wa panya wache wafanye yao.mwisho wa siku wapimane ubabe wao kwa kuwa wote sasa wamekuwa panya buku

Anonymous said...

ardhi inachimbika na kutikisika sasa escro inajulikana ilitolewa Baraka za nani si siri tena.chambuweni mtajua kizizi cha ept iptl na escrow.mwajui etc