Miji itakayoathirika ni New York City, Boston, Providence, Hartford na Portland kikubwa kilichoelezewa hapa ni upepo mkali utakaoambatana na tufani hii ya theluji watu zaidi ya milioni 28 wataathirika na tufani hii na wameonywa kutoendesha magari pasipokua na ulazima na kama itakubidi kuendesha gari basi hakikisha gari inamafuta ya kutosha, maji ya kusafika kioo na endesha taratibu huku ukikanyaga breki taratibu na hakikisha gari unalimudu katika hali hii ya theluji.
Theluji inatarajiwa kuanza leo mchana kuendelea mpaka siku ya Jumanne jioni.Safari za anga zaidi ya 2,300 zimesitishwa kutokana na tofani hiyo inayotarajiwa kuvunja rekodi.
Meya wa New York Bill de Blasio amewatahadharisha wakazi wa jimbo hilo na kuwaomba wasiendeshe magari yao kwa safari zisizokua na ulazima huku na Gavana Andrew Cuomo akiwataka wakazi wa mji huo wakiweza wafanyie kazi zao toka majumbani mwao huku akisisitiza kwamba usafiri wa umma mabasi na treni huenda ukasitisha shughuli kwa muda mpaka hapo hali itakapotengemaa.
Gavana wa Connecticut amewatahadhalisha wakazi wa jimbo hilo na kuwaambia usafiri wote wa Umma utasitishwa itakapofika saa 2 usiku. Msemaji toka Ikulu ya Marekani amsema Rais Barack Obama ambaye kwa sasa yupo ziarani India ameishwa julishwa kuhusiana na tofani hii kubwa inayotarajiwa kuanguka kuanzia muda si mrefu japo kuna sehemu kama DC, PA japo bado haijaanza kuleta madhala na tufani hii inayojulikana kama JUNO tayari imekua gumzo kila kona hususani katika majimbo haya yatakayodhurika na tufani hii.
No comments:
Post a Comment