Advertisements

Sunday, January 25, 2015

UZINDUZI WA KUTIMIZA MIAKA 38 YA KUZALIWA KWA CCM WAFANYA PEMBA


 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akihutubia wakazi wa Chake Chake Pemba kwenye uwanja wa mikutano mkongwe Gombani ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa CCM inataka kuingia kwenye uchaguzi kukiwa na amani na mshikamano,alisema"muungano wetu ndio ngao yetu" na kusisitiza Demokrasia imeanzishwa na CCM kwa kukubali mfumo wa vyama vingi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Chake Chake ambapo alitoa pongezi kwa viongozi wa CCM Zanzibar wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti kwa kufanya kazi nzuri ya kuimarisha Chama.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Ndugu Vuai Ali Vuai akihutubia wananchi kwenye sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika kwenye uwanja wa mkongwe Gombani.

 Bendi ya Brassband ya Vijana wa CCM ikitumbuiza.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Hadija Abood akisalimia wananchi waliojitokeza kuhudhuria uzinduzi wa sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM,kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Gombani,Pemba.

 Naibu Katibu Mkuu wa UWT Tanzania Zanzibar, Salama Aboud Talib akisalimia wananchi
 Wananchi wakishangilia wakati viongozi wao walipokuwa wanatoa salaam.
 Katibu wa NEC Itikadi na Unezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwasalimu wakazi waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa sherehe za kutimiza miaka38 ya kuzaliwa CCM kwenye uwanja wa mkutano Gombani.

2 comments:

Anonymous said...

wana haha wana tapa tapa maji ya shingoni.wanajua vika siku zao za kutawala visiwani zimekwisha kwisha kabisa wajitayarishe kisaikolojia kuachia ngazi na kuwapa upinzani utawala October 2015 kama hawaja iba kuraaaaaaaaa.

mwisho wa mafisadi umeshafika huko visiwani.

wapemba si wajinga tena.

Anonymous said...

wanaumeeeeeeeeeeeeeeeeeeee,wanawakeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee,ccm kwisha kwisha kabisa, ndembwe ndebwe,mlalo wa chali kifo cha mende ccm kwisha kwisha kabisa.

watapata kwa kuiba kura tu visiwani.wana hahaha.maji ya shingo.