IMAM Buhkary Islamic foundation leo imefanya kongamano la amani kwa kuwashirikisha maaskofu na wachungaji wa madhehebu ya kikristo.
Kongamano hilo linalofanyikia Hotel ya Lamada, jijini Dar es Salaam limeanza leo na litamalizika kesho, limelenga kudumisha upendo na amani kwa waumini wa madhebu yote nchini.
Katibu Mkuu wa Jopo la Mashehe Tanzania, Sheikh Hamis Mtaka alisema: “Uislam kama dini hauna tatizo na Ukristo, kwa sababu Mwislamu anautambua Ukristo na ukristo unautambua Uislam. Ambaye hautambui Uislam au Ukristo huyo anaitikadi yake binafsi na anataka kutumia dini kama kigezo cha kufanya mambo yake…tusimruhusu.
”GREDIT:GPL
”GREDIT:GPL
No comments:
Post a Comment