ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 4, 2015

WANANCHI WA KIJIJI CHA MPONDE WARUDISHIWA UMILIKI WA KIWANDA CHA CHAI

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Tanga Aisha Kigoda mara baada ya kuwasili mkoani Tanga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Tanga Mjini Omary Nundu wakati wa mapokezi yaliofanyika Segera kijiji cha Mchungwani.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mchungwani kata ya Segera waliojitokeza kumpokea akiwa njiani kuelekea Mponde jimbo la Bumbuli.
 Gari iliyombeba Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye uwanja wa mkutano kijiji cha Mponde jimbo la Bumbuli.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa Wakulima Halmashauri ya Bumbuli Almasi Kassim wakati akiwasili kwenye uwanja wa mikutano wa kijiji cha Mponde.

 Sehemu ya Umati wa wakazi wa kijiji cha Mponde waliojitokeza kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu  Abdulrahman Kinana ambaye amerudi Mponde kutimiza ahadi yake ya kurudi na kulizungumzia suluhisho la mgogoro wa kiwanda cha Chai cha Mponde.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mponde ambapo aliwaambia Serikali imerudisha kiwanda cha chai cha Mponde kwa wananchi hao.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania Mathias Assenga Benedict akisalimia wananchi wa Mponde mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,
 Mkurugenzi Mkuu wa Maendeleo ya wakulima wadogo wa chai Tanzania Ndugu Mustafa  Umande akisalimia wananchi wa Mponde.
 Mbunge wa Jimbo la Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh.January Makamba akiwasalimia wananchi wa Mponde ambapo alimshukuru Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa kazi nzuri ya kujenga na kuimarisha chama.

1 comment:

Anonymous said...

wadau hivi hiki kiwanda kilikuwa kwenye serikali gani ya Rwanda, Burundi au Somalia, leo hii kinarudishwa serikalini je kiliporwa na nani na katika nchi gani?/ mbona haya ni majanga ndani ya ndhi yetu wenyewe??