Wasichana waliokamatwa Rehema Ndunguru (32) mkazi wa Sinza akiwa na mtuhumiwa mwenzake Moyo Ramadhani
Waziri Sitta, akiondoka Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.
Waziri Sitta, akisalimiana na baadhi ya viongozi wakati alipowasili Tazara.
--
Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Samuel Sitta jana alifanya ziara Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Shirika la Usafirishaji la Reli (TAZARA) pamoja na Shirika la Usafirishaji la Reli (TRL) jijini Dar es Salaam leo.
Katika ziara yake Waziri Sitta alikutana ana kwa ana na wadada wawili wanaotuhumiwa kwa kukutwa na madawa ya kulevya walioyokamatwa wakiwa wameyameza aina ya heroini tayari kuyasafirisha kwenda mji wa hong Cong Januari 25 kwa ndege ya Emirates kutokea uwanja huo.
Wadada hao wawili Rehema Ndunguru (32) mkazi wa Sinza mpaka jana alikwishatoa pipi 78 wakati mtuhumiwa mwenzake Moyo Ramadhani alikwishatoa pipi 86 ambapo kazi ya kuwachunguza inaendelea.
Waziri Sitta alipoonana na wakina dada hao na kuwahoji hulipwa kiasi gani walisema mpaka dola za kimarekani 6500 ambazo kwa fedha za Kitanzania ni takribani shilingi 11,700,000.
Aidha Waziri alikemea wanajishughulisha na biashara hiyo chafu huku akiwaonya kamba mkono wake ni mrefu na atahakikisha anatimiza wajibu wake na sheria kuchukua mkondo wake kwa wale wote wanaoojihusisha na biashara hizo.
No comments:
Post a Comment