ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 26, 2015

Mkutano wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi Mjini Dodoma

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Chiku Galawa jana wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi unaoendelea Mkoani Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Mathias Chikawe (katikati) wakiongozana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Chiku Galawa kuingia ukumbini kwenye hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi unaoendelea Mkoani Dodoma.
Baadhi ya maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi wakiimba wimbo wa maadili ya ofisa wa polisi jana kwenye ufunguzi wa mkutano wa wakuu hao unaoendelea Mkoani Dodoma.Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi

No comments: