Stori:Na Mwandishi Wa/Risasi
MWANADADA asiyeishiwa habari, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ anadaiwa kujutia mimba yake aliyopachikwa na aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ wakati wa mapenzi yao.
Chanzo makini kilicho karibu na Wema kilieleza kwamba, mwanadada huyo kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu huku akijutia mimba aliyopewa na Kanumba ambayo ilichoropoka kwa bahati mbaya na huyo ndiye mwanaume pekee aliyewahi kumpa ujauzito.…
Mwanadada asiyeishiwa habari, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
MWANADADA asiyeishiwa habari, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ anadaiwa kujutia mimba yake aliyopachikwa na aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ wakati wa mapenzi yao.
Chanzo makini kilicho karibu na Wema kilieleza kwamba, mwanadada huyo kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu huku akijutia mimba aliyopewa na Kanumba ambayo ilichoropoka kwa bahati mbaya na huyo ndiye mwanaume pekee aliyewahi kumpa ujauzito.
“Yaani Wema anajutia kweli kwamba kwa nini hakuzaa na Kanumba kwani ndiye mwanaume pekee aliyewahi kumpa ujauzito ambapo kwa sasa anatafuta mtoto lakini hapati, yaani yupo kwenye wakati mgumu sana akikuelezea mwenyewe unaweza kulia kwani ana simulizi ya kusikitisha kuhusu maisha yake na Kanumba.
“Hii yote inatokana na kwamba kwa sasa anatamani kuitwa mama lakini hapati hivyo kujikuta akiukumbuka ule ujauzito wa Kanumba anateseka kweli moyoni,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa Wema kuhusu ishu hiyo alikiri na kuonesha namna gani anateseka moyoni.
“Nateseka kweli, tangu ilipotokea kwa Kanumba haijawahi kutokea tena. Hakuna mtu ambaye hapendi kuwa mama, nazidi kumuomba Mungu huenda na mimi itatokea nitapata,” alisema Wema.
GREDIT:GPL
1 comment:
nenda shule wewe ukasome utulize akili zako mwanamke kisomo bwana katika karne hii achaa ujinga wewe mtoto mzuri kama wewe eti unajutia mimba kupuruchuka.ujinga ujinga tu na masifa na si wewe peke yako wako kibao wasichana wenzako wanaujinga sana wakiwa na vibwana hivi na vile na misifa kibao ujinga tu,mwanamke wa kweli wa shoka anasoma anakuwa na kazi yake nzuri anatengeneza pesa MIMBA INAKUJA TU HATA UKIZIDI MIAKA 40 ASIKUDANGANYENI MTU. NINA DEMU WANGU ANA MIAKA 45 NDO KWANZA KANIZALIA HIVI SASA TENA YUPO FIT KICHWANI NA KIMWILI HANA HATA WASI WASI,THATS MY TRUE QUEEN NIMEPOA KWAKE NAJUA FAIDA YAKE.NI TAFAUTI KWELI NA WANAWAKE WENGI HANA TABIA ZA KIJINGA JINGA HATA KIDOGO SIJUI SALOON KUTENGENEZA NYWELE SIJUI KUREMBUA MACHO NA MENGI TU YAKIJINGA BABA WANGU HANAYOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO.
I LOVE YOU MY LOVELY SUPERWIFE.
Post a Comment