Wakaniambia sasa hii show ndio tunatatizo nayo kwasababu ni show ambayo inahusisha chama cha kisiasa na kama uliona hata kwenye promotion yangu nilikuwa nimeandika kuwa nitakuwa na show ya miaka 38 ya CCM Marekani, unajua vyama cha siasa hivi Chadema, CCM wanamatawi yao kule Marekani watu wanaoishi nje mara nyingi uwa wanafanya sherehe sherehe za Annivesary , kwa hiyo wakaniambia kuwa hii visa yako haikuruhusu wewe kuperform kuna aina ya Visa ya inayoruhusu msanii ku perform kwasababu show yako ni kama ya kisiasa, kwa hiyo kwa kuangalia hivyo wakaniambia option iliyopo itabidi nirudi nyumbani kwasababu shughuli iliyokuleta imeshindikana kwa hiyo unaweza ukaja mwenyewe baadae kwa matembezi yako au kwa nini lakini hata ikitokea mfano leo nikakatiwa ticket au nikate ticket nirudi Marekani visa yangu sasa hivi hainiruhusu kwa hiyo ina maana ninataka kuchukue visa nyingine yenye kibali maalumu chenye kuperform mimi kwenye show, na kama ukivunja sheria zao wanaweza wakakufungia miaka mitano halafu wanakupiga faini dola elfu 1o kwa hiyo mimi mwenyewe nikakubali lazima pia uangalie mazingira na mimi lazima nitengeneze mazingira yangu ya kazi kwa hiyo nikawaambia sawa nitarudi nyumbani kwa hiyo nasubiri tu sasa hivi wale promote wa show ya Las Vegas wapange kwaajili ya venue ya show nyingine then nitaendelea na mchakato mwingine kama kawaida.
Bofya soma zaidi uweze kumsikiliza Ommy Dimpoz mwenyewe akieleza mkasa mzima
Bofya soma zaidi uweze kumsikiliza Ommy Dimpoz mwenyewe akieleza mkasa mzima
Ommy Dimpoz: unajua kumiss flight kunatoka hata hapa Dar unaweza ukamiss flight, unajua nilishazoea kukaa kwenye zile connection za masaa matatu reporting time kwahiyo nilijichanganya kwenye masaa halafu ukishaondoka hivi inakuwa kidogo hivi masaa yanazigua kwa hiyo inabidi uwe makini kidogo kwa hiyo katika kuangalia pale yaani mimi fikra zangu na mawazo na nilishazoea zile flight za kuunganisha labda za kwenda DC unaweza ukakaa pale masaa matatu au masaa matatu na nusu kufanya connection ya kwenda lakini ile ilikuwa na connection ya muda mfupi kama lisaa limoja kwa hiyo mpaka ushuke, utoke sijui geti unalotakiwa kwenda kwahiyo katika mishe mishe nikakuta ile flight mlango umeshafungwa kila kitu wakasema haiwezekani na hata begi langu walikuwa wamelishusha kitu kingine nimeshazoea kama mule uwanja unataka watu wanatangaza kwasababu ilishawahi kunitokea mara nyingine labda unakuta abiria amechelewa flight kwasababu sisikii tangazo lolote nimekaa angani kama almost masaa tisa nafikiri nane kutoka Dar kwa hiyo nilipofika nikaunganisha wifi nikawa nimepata internet nikaingia ghafla kwenye whtsspp nasoma SMS nawaambia washikaji wa kule marekani kuwa nakuja nimeshafika Amsterdam kitendo cha pale kuchati kuwa wish watu valentine nakutana flight imeshaondoka.
‘Baada ya wao sasa kukuambia unarudi Tanzania yaani uligeuzia pale pale Airport au mazingira yalikuwaje?..
Ommy Dimpoz…;“Waliniweka Hotel kwasababu hiyo flight ilikuwa ni ya next day ambayo ni jioni mpaka zile ndege zinavyotoka huku ifike Amsterdam, ifike pale kwa hiyo ilikua ni next day…” CREDIT:MILLARDAYO.COM WA CLOUDS FM.
9 comments:
CCM New York mnaweza kurudisha pesa kama nimeamua kutohudhuria sherehe tarehe 21?
BILA YA SHAKA $40.00 ILIKUA NI YA CHKULA NA MAPAMBO TU MSANII ILIKUA NI BOUNUS
NAFIKILI HATA WAO WAMESHANGAA KUONA BADO KUNA WAJINGA AMBAO WANA FANYA MAMBO YA SIASA HUKU NJE YA NCHI YAO,IKIENDELEA HIVI ITAKUWA VIZURI KWA WAJINGA KUBADILIKA,MWENYE KUTAFUTA UONGOZI RUDI NYUMBANI UKAANGAIKIE HUKO
WADAU, HII BIASHARA YA VYAMA VYA SIASA "NYUMBANI KWA WATU" TUIANGALIE VIZURI TUSIJE TUKAJIKUTA TUNAKOSA MAMBO MUHIMU HIVI HIVI. MIMI SIJUI....
Ndio hii ni kweli, huwezi kuomba visa ya kwenda kuhubiri ccm
Pole sanaa kijana.and we love ur honesty.and for sure u will be coming again to USA kwasababu umefanya the right thing and umesikiliza sheria.kwa mbeleni ningependa nikushauri Wewe na wasanii wengine kama mnashow please muwe mnakuja mapema kama Siku mbili au tatu kabla ya show zenu; kwasababu inasaidia hata flight iki delay au bad whether you still have time to make it to were your appointment was.na pia inakusaidia Wewe kama msanii unapumzika na kuingia kwenye show fresh.kuliko unatua Leo mchana una perform usiku .hapo ndio hata show Unaona za kizembe.but I'm proud of u and we can't wait to see you soon in america.Vegas rugby itakuja tena I'm sure they will invite u or shere zao wakenya dallas.your a good person ommy.we wish u luck n well.
Rose Kachuchuru au AJ Ubao wanaweza saidia ku perform kwa gharama nafuu.
Na you watch haitaishia hapo. Mmewapa wamarekani habari kuwa kuna matawi ya vyama vyenu humu mkae mkao wa kula file lishafunguliwa na msishangae watu mkaanza kutafutwa kujieleza!! Mnalo hilo!!!
Uongooooooo...!!!😳😳😳😳😳... Dogo wacha uongo kabisaaaaa yaani wewe sema ukweli kuwa waandaaji (Junkie Promoters) hawakuwa na vibali vya kufanya shoo kwa kutaka kukwepa KODI na matokeo yake ndio hii AIBU iliyokukuta pia kuwakuta na wao pia... Kwa kifupi hawataweza tena kuleta hata wapiga ngoma sababu mapromota ni wakwepa KODI
Naomba uiachie hii comment tafadhali japo ukweli unauma.
Kila la kheri LUKE
Post a Comment